Chama cha Wanasheria Kufungua Kesi Mahakamani Kudai Kutenguliwa Kwa Miswada ya Petroli na Gesi!

Chama cha wanasheria wa mazingira-LEAT-kwa kushirikiana na wadau wa kimataifa kimepanga kufungua kesi mahakamani kudai kutenguliwa kwa miswada ya Petroli wa 2015 na mswada wa kumudu ya mafuta na gesi kutokana na kukiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 27 inayotaka rasilimali za nchi zitumike kwa maslahi ya watanzania wote.

Akizungumza na waandsihi wa habari mkurugenzi wa FOE Tanzania Dokta Rugemeleza Nshala amesema kulikuwa hakuna sababu ya miswada hiyo kupelekwa kwa hati ya dharura bila kuhusisha maoni ya wadau ambao wengine ni wataalam katika sekta hiyo na kusisitiza iwapo sheria hizo zitapishwa watanzania wataendelea kutonufaika kwa rasilimali za nchi yao kwa miaka mingi zaidi huku wawekezaji wakiendelea kuchota utajiri wa rasimali za watanzania.

Aidha wakizungumzia kuhusu rasilimali za madini baadhi ya wanasheria kutoka nchi za Afrika kusini, Togo, Nigeria, Uganda na Cameroon wamesema viongozi wanapashwa kutambua rasilimali za mafuta, gesi na madini ni mali ya wananchi wote, hivyo wana haki ya kutoa maoni yao kuhusu namna bora zinavyoweza kutumika kwa maslahi ya taifa, badala ya viongozi kufanya maamuzi binafsi bila ya ushiriki wa wananchi wote.

Chanzo: ITV
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nyinyi pamoja na hilo zee lenu penda dogodogo wote pumba tuu,mswada ushapita iliyobaki ni utekelezaji tuu.
    Mamluki wakubwa nyie,mkweeeeendreeeee

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad