EdwardLowassa ni Adui Mbaya kwa CCM Kuliko Adui Yeyote Waliyewahi Kupambana Naye

Kwenye maswala ya kiusalama na kivita huwa tunajifunza dhana mhimu sana isemayo, kumjua adui ni nusu ya ushindi. Adui wa Lowasa ni ccm chini ya "kitengo" kilichochini ya Jakaya Kikwete. Na adui wa ccm ni Lowasa.

Chadema waliumizwa mda mrefu sana na Zitto kwakuwa walikuwa wanapambana na adui wasiyemjua, siku walipomjua walimtupa nje na sasa usalama wa chadema umeimarika maradufu.

Ni bora kupambana na Adui aliyejitangaza rasmi kuwa yeye ni adui kwako kuliko yule unaekula nae na kulala nae bila kujitangaza kwamba ni adui kwako.


Lowasa anaweza kuwa adui mbaya kwa ccm kuliko adui yeyote waliyewahi kupambana nae. Kwa habari njema nikuwa majemadari wa ukombozi wakiongozwa Ally Bananga diwani wa Sombetini wamevamia kwa mikutano Monduli ilipo Ngome ya Lowasa. Habari njema zilizopo ni kwamba amevuna madiwani wa ccm na huko pia.


Ccm watapata wakati mgumu sana endapo Lowasa ataendelea kuwa mwanachama wao kuliko endapo wangemfukuza. Madiwani kumi tayari wamerudisha kadi na wanachama wengine 30,kupitia mitandao ya kijamii imeoneshwa watu wakichana chana kadi za ccm.

Lowasa ataendeleza mapambano akiwa ndani ya jahazi. Hakika litazama. Huu ni mwaka wa UKAWA kuchanga karata zao vizuri.

Mh Lowasa, nakutahadharisha, epuka mpango wowote wakutaka maridhiano na ccm, kwani mpango huo ni hatari kwa uhai wako.


Mpango mkakati huu wa lowasa ni hatari kwa ccm kuliko yote iliyowahi kutokea.

By Yericko Nyerere/JF

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lowasa hamia chadema

    ReplyDelete
  2. Ile kamati ya CCM iliyo chuja wagombea kwa kweli naipongeza kwani walitazama mbali na kutaka kuipa Inchi yao heshimakwa kuchagua mtu atakaye linda inchi na wanainchi kwa ujumla. Ila munge tereza kidogo tuu basi inchi yenu ingekua kama DRC ambayo Inchi iko kama haina viongozi. Sasa tazameni yanayo tokea hivi. Nilisema anae stahili kuongoza Inchi ni mtu wakuilinda na kulinda wanainchi sio wale wanataka faida zao binafsi. Kwa wanaojua maana ya mashindano na ushindani mnaweza nitafsiria ili nielewe vizuri. Hongera CCM, hamkutak kuuzisha Inchi yenu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad