Eti Wachezaji wa Taifa Stars Walikuwa Hawakuelewa Kingereza?, Cannavaro Atoboa Siri

Kumekuwa na headlines tofauti tofauti katika mitandao zikiwahukumu wachezaji wa timu ya ‘Taifa Stars’  kutojua lugha ya kingereza ndio chanzo iliyopelekea kutofanya vizuri uwanja na kutoelewana na aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’  Mart Nooi.


Sasa leo July 2, 2015 Nadir Haroub a.k.a  Cannavaro amefunguka na kuelezea hujuma hizo…‘Sisi wachezaji tunaumia zaidi kuliko mashabiki kwasababu maisha yetu tunategemea mpira tunapopata matokeo mabaya familia zetu zinakaa na njaa, kwanza tunakosa fedha tunazoahidiwa, tunakosa pia kuthaminiwa na watu nje unajua unapofanya vibaya watu hawawezi kukusapoti sisi tunaumia zaidi.

Kwa suala la mwalimu kusema kuwa watu hawajui kingereza sio kweli, kwani suala la mpira ni vitendo mwalimu anakuambia fanya hivi hivi na mchezaji unaelewa nini cha kufanya, matokeo yanatokea kwenye mpira unaweza ukashindwa au ukafungwa, sisi tunaumia sana na tunataka matokea mazuri ili tupate kuheshimika kwenye vilabu vyetu. Tutajitaidi na nitawaambia wenzangu to force kila game ambayo itakuwa mbele yetu tuweze kupata matokeo mazuri, sisi kwanza tunatarajia kuanzia mechi na Uganda tukishinda moja tukishinda mbili ilimradi turudishe imani kwa watanzania…’alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad