Hali ngumu ya uchumi ikamfanya Mbunge aoneshe nguo za ndani Bungeni!!

Unamkumbuka yule Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola aliyeingia Bungeni na bidhaa za kichina huku akiilaumu Serikali kushindwa kutumia rasilimali zake na kutegemea bidhaa za nje?.

Hii nyingine imetokea Zimbabwe na kuzua kizaazaa baada ya Mbunge wa upinzani Priscilla Misihairabwi kutinga Bungeni akiwa na nguo za ndani za wanawake huku akisisitiza hatma ya raia wake maskini kutokuwa na uwezo wa kununua nguo hizo.

Katika kikao chicho cha bunge kilichokuwa kikirushwa live na Televisheni ya Taifa, mbunge huyo wa Chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change ‘MDC‘ alitoa mfuko wa plastiki uliokuwa na nguo hizo.

Baada ya kutoa akamuuliza Waziri wa Fedha na sera za serikali kuhusiana na uingizwaji wa nguo hizo za mtumba  ambazo bei yake ni ndogo na husababisha madhara kwa akina mama.

Akijibu swali hilo Waziri wa Fedha Patrick Chinamasa alimtania Mbunge huyo kutokana na uamuzi wake wa kubeba nguo za ndani za akina mama lakini akasema Wizara yake  inachunguza suala hilo.

Kufuatia kitendo hicho Mbuge huyo alitolewa ndani ya ukumbi wa Bunge na wabunge wa chama tawala cha ZANU PF  kwa madai ya kutumia matamshi ya kibaguzi.

Uchumi wa Zimbabwe umedorora miaka ya hivi karibuni hali iliyosababisha viwango vya umaskini kuongezeka kutokana na kuwepo idadi kubwa ya watu wasio na ajira.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad