Hofu ya Mtoto wa Zari the Lady Boss Kufia Tumboni yatanda

HABARI ya mjini kwa sasa ni mjadala mzito mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kwamba, mpenzi wa sasa wa Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ anaweza kumuua motto aliye tumboni kutokana na tabia yake ya kuvaa viatu vyenye visigino virefu (high hills) katika kipindi hiki cha ujauzito.

WALICHOKISEMA MASHABIKI

Baadhi ya mashabiki, hasa watoto wa mjini wanaosadikiwa kuwa na mapenzi makubwa na Miss Tanzania 2006 aliye pia nyota wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu (Team Wema), ambaye aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond, wamemnanga Zari wakisema kuvaa kwake high hills ‘kokoko’ kunaweza kumminya tumbo wakati wa kutembea hivyo kukifanya kitoto hicho kufia tumboni.

DOKTA AZUNGUMZA, AFAFANUA

Kufuatia madai hayo mazito, juzi Amani lilizungumza na daktari maarufu jijini Dar, Godfrey Chale ‘Dokta Chale’ ambaye alilazimika kueleza kuhusu madai hayo.

Amani: “Samahani dokta, tumelazimika kukutafuta kutokana na maneno yaliyosambaa kwa sasa hapa mjini. Diamond ana mpenzi wake ni mjamzito. Sasa pamoja na ujauzito wake, anavaa viatu virefu.

“Kwa hiyo wanamnanga kwamba anaweza kukiua kitoto kilichopo tumboni kwa sababu anapovaa viatu hivyo, misuli ya

miguu inakaza na anabana tumbo. Kuna ukweli?”

Dokta: “Kwanza kabisa siyo kweli. Mwanamke anapovaa viatu virefu wakati wa ujauzito hakusababishi mtoto tumboni kufa.

“Ila, inashauriwa wajawazito

wasiwe wanavaa viatu virefu kwa sababu, wanapovaa, wanatanua misuli na kujiongezea uzito. Kwa hiyo inakuwa kama mtu aliyebeba mzigo kichwani huku akiwa na mimba.”

ATAJA MAGONJWA YANAYOMKABILI ZARI

Dokta Chale aliendelea kuweka wazi kuwa, mjamzito anapopendelea kuvaa viatu virefu, akishajifungua na mwili ukapoa, atakabiliwa na magonjwa manne.

“Kwanza ataugua miguu. Pili, atasumbuliwa na matatizo kwenye visigino. Tatu atapata matatizo ya magoti na nne ataugua mgongo. Ndiyo maana unaweza kukuta mwanamke anakuwa mrembo, miguu mizuri lakini kama alikuwa akibeba mizigo au kuvaa viatu virefu wakati wa mimba, miguu inaota nyama kwa nyuma ‘kiazi’.”

AONDOA HOFU

“Kwa hiyo, kama jamii ina hofu kwamba huyo mjamzito atamuua mtoto aliye tumboni kwa sababu ya kuvaa viatu virefu, hofu hiyo iondoke bali yazingatiwe hayo matatizo manne niliyoyasema,” alisema daktari huyo.

KWA WANAWAKE WOTE

“Lakini madhara haya si kwa wajawazito tu. Utafiti wa kitaalam umegundua kuwa, mwanamke ana uwezo wa kutembea wastani wa hatua 10,000 kwa siku. Kwa hiyo kuvaa viatu vyenye visigino virefu hufanya nguvu inayotumika kutembea hatua moja kuwa kubwa zaidi. Sasa utaona madhara ya kutembea hatua 10,000. Hii haijalishi anayetumia gari.

“Matokeo yake husababisha misuli na mishipa ya kwenye miguu, kiuno, mgongo na shingoni kufanya kazi kubwa ya kujaribu kusawazisha uzito. Kazi ambayo kwa kawaida hufanywa na visigino,” alimalizia dokta huyo.

DIAMOND ALIVYOSEMA

Amani, juzi lilimtafuta Diamond kwa njia ya mtandao wake wa WhatsApp na kumuuliza anachukuliaje madai ya ‘wabaya’ wa Zari:

“Hao wapo tu. Unajua dunia hii ukishakuwa maarufu kila jambo litakuandama. Lakini mimi naangalia mbele zaidi, nini nafanya na nini nitafanya. Kama maneno hata kwenye kanga yapo.”
GPL

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mnakosaga vya kuandika au?kama wase....,zari zari mfuuuuuu.

    ReplyDelete
  2. Guys, you have to stop that. Marekani hapa watu tunavaa viatu vilefu mpaka tunaenda labor. Let the lady enjoy her pregnancy duuu watanzania bwana. why cannot you mind your own business?

    ReplyDelete
  3. Afu nyie wanafiki sana mmejuaje ni team wema hebu mpumzishen mtoto wa watu mnapoongelea mambo ya huyu kunguru msimuhusishee

    ReplyDelete
  4. mna laana nyie watanganyika,kuanzia waandishi wa habari na raia kwa ujumla,yaani kwaombea watu mabaya tu hamna jingine, kama hamna habari za kuandika msiwazushie watu mambo ili muuze vigazeti vyenu,yaani laana tupu mko soo negative na mambo ya watu tena wengine mtakuta mmefunga kabisa,mashetani kweli nyie sasa akifia tumboni ndo mtafurahi?kuna habari nyingine aibu ata kuziandika kwa taaluma ya mwandishi wa habari.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad