Gazeti la Mwananchi la Jumatatu, Julai 27, 2015, kwenye ukurasa wake wa 26 limechapisha habari yenye kichwa cha habari, “Marais watano wanaotajwa kuongoza kwa mishahara minono barani Afrika ni hawa hapa”.
Katika habari hiyo ambayo gazeti hilo linadai chanzo chake ni “uchambuzi wa mtandao wa African Review” inadaiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, anashilikia nafasi ya tano miongoni mwa viongozi 38 wa nchi za Afrika wanaolipwa mshahara mnono zaidi.
Gazeti hilo linadai kuwa Rais Kikwete analipwa Dola za Marekani 192,000 kwa mwaka, ikiwa ni malipo ya Dola za Marekani 16,000 kwa mwezi.
Habari hizi siyo za kweli. Ni uongo na uzandiki. Ni uzushi mtupu na ni uzushi wa hatari.
Mshahara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwezi ama kwa mwaka haufikii na hata wala kukaribia kabisa kiwango kinachotajwa na Gazeti la Mwananchi.
Tangu Uhuru, mwaka 1961, Rais wa Tanganyika na baadaye tangu mwaka 1964 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekuwa miongoni mwa viongozi wanaolipwa mishahara ya chini kabisa duniani.
Mshahara wa Rais wa Tanzania kwa mwezi ni wa chini kiasi cha kwamba mshahara wake unazidiwa, tena kwa mbali, na mishahara wanayolipwa baadhi ya watendaji wakuu wa baadhi ya taasisi za umma nchini.
Aidha, ni jambo la kushangaza kwamba Gazeti la Mwananchi, linalochapishwa hapa nchini, linaweza kupata kiasi cha uongo anacholipwa Rais wa Tanzania katika mitandao ya nje badala ya kuuliza rasmi na kupewa majibu sahihi.
Kwa kujiingiza katika uzushi wa kupindua kiasi hiki, Gazeti la Mwananchi haliwezi kuwa na nia nyingine yoyote isipokuwa nia ya kuwachochea wananchi na kuwajengea chuki dhidi ya Serikali yao na Kiongozi wao Mkuu.
Ni matarajio yetu, kuwa Gazeti la Mwananchi litafanya jitihada za makusudi, kama taaluma ya uandishi wa habari inavyoelekeza, kutafuta usahihi wa jambo hili na kuwaambia Watanzania ukweli.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
27 Julai, 2015
IKULU Yaukana Mshahara Wa Rais Kikwete........Yasema Gazeti La Mwananchi Limepotosha
3
July 28, 2015
Tags
Nyinyi serikali mnayalea hayo majarida,hilo mwananchi ni gazeti la kenya limeweka watu wake hapa tz,fukuza tuuu.
ReplyDeleteSasa kama gazeti mwananchi limedanya mshara wa Raisi na nyie mnasema ni wa kiwango cha chini sana Kwa nini msingekitaja hicho kiwango kama si mnataka kuufunika ukweli. Anyway, watanzania tumeshajua ukweli wa nchi maskini kama tanzania inamlipa Rais wake mapesa yote hayo kama nchi Tajiri nawakati wananchi wake wanakufa Kwa umaskini wa kila aina kila siku..........ukweli tumeuelewa na tutaendelea kujua mengi tu...... mjue sisi wananchi twawaweka kiporo tu nyie serikali iko siku tutawatawanya wote vichwa vyenu.......
ReplyDeleteSeem I kiasi gani tujuwe
ReplyDelete