#TAHADHARI! Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Jeshi la Polisi, Tanzania Human Rights Defenders, Tawla, Wlac, Legal Human Right Center, Wildaf, Tume ya Haki za Binadam, Tamwa, Tgnp, Wananzania wote wapenda Maendeleo ya Halali, msaidieni huyu Mwanaharakati aliyethubutu Kujitosa mithili ya Swala katikati ya msitu ulojaa Simba wenye njaa, Mpiganaji wa kweli aliyejaaliwa Kipawa cha kusema bila kumumunya, ambae amejitokeza kupigania Haki za Binadamu kwa kupiga vita Madawa ya kulevya nchini mwetu!!
Kiukweli @mangekimambi_ Amejitosa upande ambao wengi wetu tunaojiita "Wanaharakati" tumeufumbia macho na tunaogopaaaaa kuwanyooshea vidole wanaohusika kwenye mtandao huo 🙌 Ila huyu Bi @mangekimambi_ Ni mtanzania pekee alieamua kujitoa Sadaka kwa ajili ya Watanzania wenzake hususan vijana wanaoangamia kwa kubwia unga au madawa ya kulevya kila kukicha....
Huyu @mangekimambi_ naona ana uthubutu wa hali ya juu mno katika kukemea maswala mbalimbali kwa maslahi ya wengi hasa Taifa likiwepo la madawa ya Kulevya, na hivyo kuhatarisha uhai wake. Kwa sasa ametangaza kutishiwa Uhai kwenye accont yake ya Insta kwamba kashikiwa BASTOLA jambo ambalo halipaswi kufumbiwa macho kabisa...
Kama kweli tunaipenda nchi yetu basi ni wakati wa kuwalinda Wanaharakati wanaojitokeza kuokoa kizazi cha vijana na Taifa hasa pale wanapojaribu kukemea uovu na kukumbwa na changamoto kubwa kama hiyo ya kutishiwa kuondolewa Uhai wao... Tusisubiri mtu auliwe ndo tuanze kutoa salam za pole bali tuchukue Tahadhari mapema...
Binafsi Nikijaribu kuvaa viatu vya kina RayC, Banza, na wengine wengi nadata na nazidi kukuombea Bi @mangekimambi_ Mungu akulinde kwenye hayo Mapambano maana yeye pekee ndo Mtetezi na Mtenda Haki Milele...
Nimeumizwa sanaaaaaa ila ndo ivo nchi hii tunawatukuza wanaopata pesa kwa kuangamiza watu wengine
JOYCE KIRIA: Jamani Tumsaidieni MANGE KIMAMBI Mwanaharakati Aliyethubutu Kujitosa Mithili ya Swala Katikati ya Msitu Ulojaa Simba Wenye Njaa, Mpiganaji wa kweli Aliyejaaliwa Kipawa cha Kusema Bila Kumung'unya
10
July 17, 2015
Tags
Akome si anajifanya mjuaji mwambie aache kutukana watu alimwandama Zari dada wa watu kimya Na hali yake ya ujauzito wala hajali mwenzie hata mimba ingeweza kutoka Na yeye anajua mtu akiwa mjamzito anakuwa Na hali gani,Leo hii asaidiwe akae huko apate fundisho
ReplyDeleteKupapmbana Na madawa ya kulevya sawa ila aache kuingilia maisha ya watu binafsi anawanynyasa Sana watu kisaikoljia kwa mfano anavyomsakama baba wa watu Lowasa Na ugonjwa wake daah! Amseme kwa ufisadi lakini si ugonjwa Na Kuna njia nzuri ya kuelezea huo ugonjwa lakini yeye anavyowaslisha Kama vile huyo baba aliomba huo ugonjwa,wote waliotukanwa waende huko polisi akome Na wale wanaompa kichwa wakamsaidie sasa!
ReplyDeletewell said
DeleteMange ungesubiri makufuli achukue nnchi kwanza.kama raisi anawajua na amekaa kimya Wewe ni Nani?umeniliza ulivyosema. "I think i would rather die than live without a purpose" my dear u my hero already. Mungu awe Nawe.
ReplyDeletehero??? acha ujinga wewe unaelewa maana ya hero?? kama huna cha kuandika uwe unakaa kimya
DeleteMANGE MTANDAO HUO NI MKUBWA MNO NGUVU YAKO PEKEE HAITOSH HUTAWEZA WATAKUUA BURE ITABAKIA SIMULIZI .NENDA ULAYA KWAKO KAFANYA MAMBO YAKO.KUNA DADA MMOJA MPAMBANAJI SANA ALIKUWA ANAITWA BETTY . ALIKUTWA KWENYE MTARO AMEUWAWA. MIMI NAKUPENDA MANGE ACHA LABDA USHIRIKIANE NA VIONGOZI WALIO JUU
ReplyDeleteWELL DONE JOYCE KIRIA.
ReplyDeleteTATIZO VITA HII WENGING WANAIOGOPA NA WAKATI NYINYI MEDIA NDIYO MNATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE.
Niukweli mtupu nahata mimi najua kama huyu kaka anauza unga na anatumia power ya serikali kutishia watu na ushahidi ninao. Tunasubiria tu afunguliwe kesi yaye na kundi lake. Ana kundi laki ambalo lina mprotect wake ambao wanaend
ReplyDeletehiyo issue ya madawa ya kulevya amuulize Amina Chifupa yuko wapi sasa? Anawajua wenye huo mtandao utakufa hivi hivi unaona endeleza harakati kazi kwako
ReplyDeleteHakuna atakae ishi milele Amina chifupa alikufa na mimi nitakufa mange atajufa hata wewe na wauza sembe wote watakufa, haogopwi mtu na haki itatendeka, kuna p rofesional lawyer washa shikilia kesi kitaeleweka tu mwaka uuu ALUTA CONTINUE HATUOGOPI KUFA.
ReplyDelete