Kajala Afungukia Kuingia Kwenye Siasa

Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ amefungukia kuingia kwenye siasa kuwa ni bora abaki kwenye upenzi na chama fulani kwani hawezi kugombea.

Akizungumza na Amani juzikati, Kajala alisema kuwa, japokuwa wasanii wengi wakiwemo wa tasnia ya filamu Bongo, wamekuwa wakichukua fomu za kutaka kugombea nafasi mbalimbali za udiwani na ubunge lakini kwake hafikirii kitu kama hicho.

“Mimi siasa siiwezi kabisa, kifupi haipo kwenye damu ndiyo maana unaona wenzangu wote wamechukua fomu za kugombea mimi wala sijajitokeza kuchukua,” alisema Kajala.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad