Kikwete: Wasanii wa Bongo Fleva wanatuliwaza kwa kuitangaza Tanzania pale tunapofanya madudu kwenye soka

Rais Jakaya Kikwete amesema wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wameipeleka Tanzania mbali kwa kazi nzuri wanayoifanya na hivyo kuwaliwaza watanzania kwakuwa nchi bado inaendelea kufanya ‘madudu’ kwenye soka la kimataifa.

Akihutubia bunge mjini Dodoma jioni hii, Kikwete amesema wasanii wanaliletea taifa heshima kubwa hivyo ni lazima wawezeshwe zaidi.

Rais Kikwete amedai kuwa kwa kutambua umuhimu wa sanaa nchini, aliamua kuwaleta watu mashuhuri katika muziki nchini Marekani akiwemo mtangazaji wa E! News, Terrence J, meneja wa Ludacris, Shaka Zulu na producer David Banner ili kuja kuwapa elimu wasanii wa nyumbani.

Ameahidi kuwa atafanya mpango wa kuwaleta tena kwaajili hiyo na pia kutumia muda aliosalia madarakani kufanya awezalo kuwasaidia zaidi.

Wasanii mbalimbali akiwemo Diamond Platnumz wametoa maoni yao kuhusiana na kauli huyo.


  • “Hakika Mh Rais @jmkikwete alitukuta kuleee…sasa anatuacha hapa palipo juu zaidi…Dah! Daima tutakukumbuka kwa mengi mema uliyotufanyia,” ameandika Diamond kwenye Twitter.


Naye Shilole ameandika kwenye Instagram: Wasanii wanatupa heshima! Wanatupunguzia hasira za soka! Nimekupenda bureee mh rais tishaaaaaaaaaaaa.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad