William Malecela, maarufu kama Lemutuz Nation au "King of All Bongo Social Networks" kama anavyofahamika katika mitandao mbalimbali ya kijamii ameeleza sababu za yeye kutosomeshwa na baba yake mzazi.
Le Mutuz Nation ambaye ametumia muda mwingi kusoma na kuishi nchini Marekani na Belgium, ameweka bayana katika kipindi cha Mlimanidotcom cha Mlimani TV kuwa alijisomesha kwa kupitia fedha ambazo zilitokana na kazi mbalimbali ambazo alikuwa akifanya kama vile udereva wa mabasi makubwa huko jijini New York pamoja na kukaanga kuku.
Alipoulizwa kuhusu taarifa za yeye kujisomesha kupitia kuendesha malori na kukaanga kuku, Le Mutuz alisema “Liko sawasawa, unajua ni la ajabu Tanzania lakini si la ajabu nchi nyingine kwasababu mimi wakati nakua, tulikuwa kwenye siasa ya ujamaa kwa hiyo mambo mengi yalikuwa yamebana na mimi nilikuwa nataka ubaharia”
Alieleza kuwa sababu kuu ni kuwa yeye alitaka ubaharia lakini baba yake hakutaka yeye asome masomo hayo katika ngazi ya chuo kikuu, Lakini pia ameeleza kuwa baba yake ambaye ni Waziri mkuu wa zamani wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hakumsomesha kwasababu kipindi yeye anakua ilikuwa ni kipindi cha ujamaa na mambo mengi yalikuwa yamebana hivyo baba yake asingeweza kumlipia kusoma nje ya nchi.
Pamoja na kueleza hayo, Lemutuz alizungumzia sababu za yeye kuliburuza gazeti la Kiu mahakamani na pia kwanini anapenda kupiga picha na wanawake na kuweka Instagram
na mi nilikuwa najiuliza kama lemutuz ni mtoto wa malechela mbona hampigii debe dada yake mwele anazungumzia wengine tuuuu?
ReplyDeleteHuyo na Dr. Mwele wanashea baba, huyo mtoto wa nje ya ndoa so ule ukaribu na wakina dr haupo hawezi kumpigia debe
ReplyDelete