LINAH SANGA: Nimempata Mwanaume wa Ndoto zangu, Alinikuta Nikiwa kwenye Maumivu ya Mapenzi

Linah Sanga amedai kuwa amempata mwanaume aliyekuwa akimtafuta kwa muda mrefu na alikuja katika maisha yake muda aliokuwa ameumizwa kimapenzi.

Akizungumza na Bongo5 leo, Linah amesema mwanaume aliye naye kwa sasa ni mwanaume aliyekuja kumuokoa akiwa katika wakati mgumu wa kimapenzi.

“Kiukweli malengo yetu ni ndoa na wala haitachukua muda mrefu. Mungu akijalia mwakani,” amesema Linah. “Sasa hivi nataka ndoa mambo ya kuzini sitaki. Mimi sidhani kama ndoa ina ugumu wowote. Nataka sasa hivi kuwa wa halali kwa mtu mmoja na baadaye tupate watoto. Kwa jinsi tulivyoongea kazi ni kazi na mapenzi ni mapenzi, kwahiyo nafasi yangu ya kazi itakuwa pale pale. Na ninafikiri huyu ni mtu sahihi kwangu, ninafikiri ni mtu ambaye anaweza akawa mume wangu ndio maana nimekimbilia ndoa,” ameongeza.

“Amekuja kwangu kama mtu anayenipenda, ameona jinsi ninavyoumia kimapenzi. Kwahiyo huyu amekuja kama mtu mwenye nia, ni aina ya mwanaume ambaye nilikuwa namtafuta kwa muda mrefu na hatimaye amefika, sasa hivi nafurahi.”

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jitangaze tu mama usiusemee moyo hujui ana waza nini kwako ni kumuomba mungu na iwe kweli na ndoa mfunge ile ni vyema ungepiga kimya sio kutangaza.

    ReplyDelete
  2. Kila siku mnasemaga hivo skumbili umeachikaaa Hahahaaaaaa usipojipanga atakupanga

    ReplyDelete
  3. LINAH NGOJA NA WEWE UINGIZWE KWENYE MTANDAO WA WAUZA SEMBE

    ReplyDelete
  4. HAHAHAHAAHH MNAJUANA NYIE HULKA ZENU ZINAENDANA.
    MUHAYA MUGANDA \WALITENGANISHWA NA MPAKA TU.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad