TETESI:Lowassa Aandaa Waraka Kumchanachana Kikwete, Kisha Kutimkia Ng'ambo...

Hatimaye mbunge wa Monduli Edward Lowassa kesho atatoa waraka mzito utakaoelezea namna ambavyo alifanyiwa kile alichokiita 'hila' na rais Kikwete.

Waraka huo unatarajiwa kulitikisa taifa na huenda ukaigawa vibaya CCM.

Baada ya waraka huo pia Edward Lowassa anatarajiwa kutoa rasmi hatima yake kisiasa huku kila dalili ikionyesha kuwa ataisambaratisha vibaya CCM kutokana na maamuzi atakayochukua.

=======
UPDATES:

- Miongoni mwa mambo mazito yaliyo kwenye waraka huo ni hatua ya Edward Lowassa kumuunga mkono Dr. Willbrod Slaa kama mgombea urais anayekubalika na wengi baada ya yyeye kuenguliwa.

- Pia kuna dalili (ingawa siyo za wazi na zimetawaliwa na giza nene kwamba huenda Lowassa atatangaza rasmi kuhamia Chadema ingawa hatagombea urais).

- Taarifa nyingine zinabainisha kuwa EL baada ya kubwaga manyanga, atatimkia ng'ambo wakati CHADEMA wakimwandalia mapokezi "mazito"

By G Sam

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Asie kubali kushindwa sio mshindani Lowasa jua ulivoamini wewe Mungu alipanga tofauti na kusudi la Mungu haliwezi kupangwa na wanadamu hapo unatafuta adhabu toka kwa Mungu kwa hiyo una mrekebisha Mungu kuwa amekosea kuchagua kumbuka kua Mungu haangalii pesa za mwanadamu kwa maana Mungu mwenyewe nitajiri akiamua hata hivo ulivonavyo atakunyang"anya tunaomba kwa ajili ya Taifa natuna muombea magufuli Mungu amfanikishe hata ukihama ndo unaendelea kutangaza ufisadi kama pesa zako umekosa sehemu ya kupeleka wape watoto yatima ziwasaidie watu wachache wanakupa kichwa na hawatakusaidia chochote alicho panga Mungu mwanadamu hawezipangua kaa utafakari vizur

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad