Lowassa: Harusi Yageuka Matanga Mbio za Urais

Tumeshuhudia mbuyu ukichinjwa kwa wembe na kuanguka chali. Hii ni tamthiliya ya 4U Movement iliyoratibu project ya kumuingiza Lowassa Ikulu ya Magogoni.

Wadadisi wa mambo wamekuwa na maswali yasiyojibiwa hasa kuhusu ULAZIMA wa kuhakikisha Lowassa anapitishwa na chama chake kwa gharama zozote. Swali lingine ni tija ya projekti nzima kwa Watanzania...

Je waliohusika na mradi huu wanarandana na haiba ya mtu wao? Hapa nazungumzia watu kama Apson, Kingunge, Rostam, Chenge, Nchimbi n.k.

Je chaguo la Watanzania ni chaguo lao? Au chaguo lao ndilo chaguo la Watanzania?

Udadisi hauishii hapo bali plan B ya Wezesha Lowassa na utiifu wa kundi lake kwake nk.

Tambo za Lowassa kuwa hakuna wa KUMKATA jina lake kwenye hatua zote za mchujo, ni wazi kuna egemeo thabiti la ndani ya chama alilokuwa amejiaminisha kwake. Inawezekana mtaji wa wajumbe wa NEC na hamasisho la wajumbe wa mkutano mkuu, inawezekana vilimpa imani kuwa ana kundi kubwa linalomuunga mkono.

Tangu mteule wa CCM kupatikana, Lowassa amekuwa kimya kumuunga mkono au kukosoa mfumo uliofikisha utimilifu wa mchakato mzima. Hivyo haiyumkiniki plan B inaweza kuleta kishindo ama maumivu zaidi.

Shamrashamra, majivuno na tambo za mashabiki wa Lowassa ambapo walithubutu kutumia CCM kama kichaka chao hata kukiuka taratibu, kanuni na maadili ya Chama kwa kigezo cha kupendwa vimegeuka simanzi na fadhaa nzito kwao.

Hakuna tofauti na msiba kugeuka matanga na historia haibadilishwi...

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. INATOSHA,AU MMETUMWA?MMALIPWA NA NYINYI?

    ReplyDelete
    Replies
    1. IMEKUUMASANA AMA NN? MBN HUELEWEKI AU NA WEWE NI MSHIRIKA WAKE? HAAAHAAAA NICHEKE MIE, ETI KAKATWA INA MAANA TANGU UTOTO WAKE ALIKUWA HAJAKATWA? MAZITO YA KABWE

      Delete
  2. wampe tenda yab mradi wa karatasi za kupigia kura na masanduku ili arudishe pesa zake alizokua anagawa kama njugu

    ReplyDelete
  3. WASWAHILI WALISEMA KUWA KUTESA KWA ZAMU

    ReplyDelete
  4. WASWAHILI WALISEMA KUWA KUTESA KWA ZAMU

    ReplyDelete
  5. Matokeo ya FORM 6 yametoka,hebu tuwekeeni hapa.
    Lowasa,lowasa,tumechoka sasa.

    ReplyDelete
  6. Ikulu Ni mahali patakatifu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad