Lowassa: Je, Alikosea Wapi? Akiamua Kuendelea, Arekebishe Wapi?

Mchakato wa kutafuta mgombea urais kwa tiketi ya CCM umeshakamilika, na mgombea aliyepatikana ni John Pombe Magufuli. Pamoja na hayo, ukweli unabakia kwamba katika mchakato wa kutafuta wadhamini, ni Edward Lowassa ndiye aliyeungwa mkono na wanachama na makada wengi wa CCM kuliko mgombea mwingine yoyote.

Edward Lowassa aliungwa mkono na wanachama karibia milioni moja wa Chama Cha Mapinduzi. Pamoja na jina la Edward Lowassa kutorudishwa na vikao vya ngazi za juu ya CCM, kuelekea uchaguzi mkuu, suala la Lowassa kupata wadhamini karibia milioni moja ni suala ambalo halitakiwi kuchukuliwa kimasihara au kubezwa, kote - ndani na nje ya CCM. Kwanini tunasema hivyo:

1. Wadhamini hawa karibia milioni moja ni mchanganyiko wa wanachama na viongozi wa ngazi mbali mbali wa CCM. Wanatoka katika kona mbalimbali za Tanzania. Ni hawa ambao kwa kawaida, ndio wanaochukuaga jukumu la kumbeba na kumnadi mgombea urais (CCM) baada ya jina la mgombea kupatikana.

2. Kwa kuzingatia historia inavyotueleza, upinzani umeweza kunyakua makada wengi wa CCM baada ya makada hao kuenguliwa majina yao na vikao vya juu vya chama, licha ya makada husika kukubalika na kuwa chaguo la wanachama na makada wengi wa ngazi za chini. Kilichofuatia ni kwamba, CCM ilikuja kupoteza majimbo kadhaa kwa upinzani.

Kama ilivyotokea huko nyuma kwa makada kadhaa kuenguliwa katika vinyang’anyiro cha ubunge hivyo safari yao ya matumaini kuzimishwa na vikao vya juu vya CCM licha ya kukubalika na makada wengi wa ngazi za chini za CCM, hali hii imejitokeza kwa mara ya kwanza katika kinyang’anyiro cha kutafuta mgombea urais (CCM) ambapo, Safari ya matumaini ya Edward Lowassa kubeba bendera ya CCM (urais) 2015, Safari hiyo imezimwa rasmi na vikao vya juu vya chama cha mapinduzi. Je:

· Edward Lowassa alikosea wapi katika safari yake ya matumaini ndani ya CCM?

Na iwapo itatokea akashawishika kuendelea na safari yake ya matumaini kupitia chama kingine cha siasa kama ilivyotokea kwa makada wengine walioenguliwa kwenye vinyang’anyiro vya ubunge (CCM), ili kutimiza safari yake ya matumaini nje ya CCM, je:

· Edward Lowassa arekebishe wapi ili kufika safari yake ya matumaini nje ya CCM?

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Iwapo atafanya hivyo, ni kueleza ukweli woote wa anachokijua ndani ya ccm yaani uovu wote wa ccm juu ya taifa hili na kutueleza ukweli wote juu ya sakata la richmond. Hapo safari ya matumaini itakuwa salama kwake maana atarudisha imani ya wananchi juu yake. Ila simshauri kufanya hivyo maana atapambana na mitikisiko mingi kutoka ccm.

    ReplyDelete
  2. Aongeze dau, alilotoa safari hii ni dogo!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. aisee we unafaa kuwa waziri mkuu , tutaendelea =))

      Delete
  3. Mwandishi sikiliza! Kujiuzulu kwa makosa halafu ukarudi kuomba tena ridhaa ya waliokutoa kukuweka huoni kwamba inahitaji labda Mungu awe amesema? Mzee wetu anawakati mgumu sana na tunashindwa kumshauri kitu kitakacholeta matokeo chanya. Ukweli kupata nafasi ya urais kwake ni ngumu sana labda kimiujiza tu. anawajua CCM ndani na nje na akienda mahali pengine atatumia kama rungu na hilo anaweza hatarisha maisha yake. Namwomba mzee wetu atafute namna ya kwenda bungeni maana utendaji wake bado tunauhitaji hata katika nafasi ndogo kama hiyo. MUNGU IBARIKI TZ

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad