Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa alitambulishwa rasmi kuhamia CHADEMA July 28 2015 Dar es Salaam akiwa ameongozana na mke wake, Regina Lowassa pamoja na watoto wao.
Kwenye Orodha ya Viongozi wa UKAWA ambao walikuwepo kumpokea na kumkabidhi kadi ya CHADEMA, alikuwepo James Mbatia, Prof. Lipumba, Dk. Emmanuel Makaidi, Salum Mwalimu na Freeman Mbowe.
Salum Mwalimu ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, jana alisema haya kuhusu mapokezi hayo;
"Tunashukuru sana Watanzania, sidhani kama kuna kiongozi wa CHADEMA simu yake iliwahi kuzidiwa kama jana, simu zilizidiwa kwa pongezi… Kila mtu amezungumza kwa sababu ya Historia ya tendo lenyewe.
"Kesho(LEO) Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa atachukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA… pengine kutakuwa na shamrashamra nyingi itategemeana na Mgombea mwenyewe, akiamua kuja na mdundiko haya… lakini tunaamini kutakuwa na shamrashamra nyingi."
Salum Mwalimu pia alizungumzia sababu za viongozi wengine wa UKAWA kutokuwepo( Tundu Lissu na Dr. Slaa) ambapo alisema;
"Tuna mambo mengi tuna mikakati mingi, tumegawanyika… sio kila tukio wote tuwe pamoja.
"Jana mliuliza Tundu Lissu yuko wapi na leo huyu hapa hata hamumuulizi… Tuko kwenye kipindi cha Uchaguzi,tuna mambo mengi hatuwezi wote kuwa sehemu moja, tunagawanyika kutokana na ratiba tuliyonayo."
LOWASSA Kuchukua Fomu ya Kugombea Urais LEO kwa Mbwembwe na Shamrashamra!!
0
July 30, 2015
Tags