Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimemtaka mwanasiasa mkongwe, Kingunge-Ngombale Mwiru kufanya anachotaka kufanya.
Juzi Kingunge alijitokeza hadharani na kuzungumzia na waandishi wa habari huku akiwaambia kwamba kilichofanywa na CCM katika kumpata mgombea wa urais, Dk. John Magufuli ni haramu.
Dalili ya CCM kupasuka vipande zimeanza kuonekana dhahiri, baada ya Kingunge kujitokeza hadharani kupingana na maamuzi yote yaliyofanywa hususani kukata jina la Edward Lowassa katika hatua za mwanzo za kuteua mgombea urais.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (pichani), akizungumza na mtandao huu jana kuhusu tuhuma zilitolewa na Kingunge ambaye kadi yake ya uanachama ni namba nane, alijibu kwa kifupi kwamba afanye anachotaka kufanya na kwamba hana maoni zaidi.
“Sina Comment (maoni) wewe unataka niseme nini? kaandike hivyo nilivyosema kwa sababu na mimi ni mwandishi na nilishawahi kuwa mhariri kwa hiyo najua,” alisema na kukata simu.
Chama hicho tawala kilimteua Dk. John Magufuli na Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wake mwenza kupeperusha bendera yake katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwakani.
Jumla ya watia nia 38 majina yao yaliingia katika vikao vya awali, lakini waliovuta kuingia tano bora ni Magufuli, Dk. Asha-Rose Migiro, Balozi Amina Salum Ali, Januari Makamba na Bernard Membe.
Hata hivyo, Halmashauri Kuu (NEC) iliwachuja Makamba na Membe na kuwabakiza Magufuli, Amina na Migiro kisha Magufuli kuibuka mshindi
umefutika katika siasa za kistaarabu dikteta mkubwa ila kosa tunamlaumu mbwa badala ya mwenye mbwa
ReplyDeleteItisheni Halmashauri Kuu kumfukuza kama hamtafukuzwa nyinyi??
ReplyDelete