Maneno 36 ya Waziri Membe Kuhusu Mtu Aliyekamatwa na Mabilioni ya Wajumbe Dodoma..

Kuna stori zimeenea mitandaoni kwamba kuna mtu ambae amekamatwa na mabilioni ya pesa Dodoma, kingine ni kwamba amekamatwa na simu ikiwa na maelekezo kwamba pesa hizo ni za kuwapatia Wajumbe.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ameandika ujumbe @Twitter kukanusha kuhusika na mtu huyo

  • “Kuna taarifa za uongo zinazoenezwa kwamba kuna “Mtu wa Membe” amekamatwa na pesa Dodoma“


Kwenye Tweet nyingine Waziri Membe ameandika hivi

  • ”siasa hizi ni za hovyo kwani hazitajenga Taifa letu. Naomba msihadaike na watu wanaotaka kututia doa baada ya kukosa uchafu dhidi yetu”  @BernardMembe

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Siasa ni mchezo mchafu kama wahenga walivyosema. Na uchafu wenyewe unakuja kwa kuwa wanasiasa waliowengi ni wachafu.

    Uchafu wa wanasiasa uko katika maeneo mengi. Uadilifu wa wanasiasa wengi katika nchi za Afrika ni wakutilia shaka. Walio wengi wanajilimbikizia mali na kufanya mambo ambayo yatahakikisha wanapata ulinzi baada ya wao kuondoka madarakani.

    Wengi wao ili kutimiza azma hizo , hufanya kila mbinu ili kuwaweka vibaraka wao ambao nao hata hivyo huwa ni wezi na wenye hulka nyingi za kiimra ili kuendelea kuwa salama baada ya maovu yao wakiwa madarakani.

    Baadhi yao hurithisha watoto wao ili kuhakikisha wanabaki salama wakati wote kabla kifo hakijawafikia. Hizi ndizo siasa za nchi nyingi maskini duniani ambazo huwa na viongozi matajiri wa viwango vya matajiri wa ulimwengu wa kwanza wakati wananchi wao wanatembea bila hata nguo au mlo wa siku.

    Hali kama hizi husababisha baadhi yao hata kubadili katiba halali za nchi zao ili kuongeza vipindi vya kuendelea kuwepo madarakani. Hii ni hatari kwa mistakabli ya kiuchumi na maendeleo ya jamii nzima ya Nchi husika.

    Hata Tanzania yetu ambayo inasifika duniani kote kwa amani na utulivu inakabiliwa na majanga ya maovu ya wanasiasa ambao wana kila nafasi ya kufanya maamuzi ikiwa ni pamoja na kutunga sera na sharia mbalimbali zinazotumiwa na jamii nzima.

    Watunga sharia wa namna na hulka za uchafu wa viongozi wa afrika hushiriki na kuweka mashinikizo makubwa kuhakikisha sharia na sera dhaifu zinapitishwa ili kuacha mianya ya kuiba na kuendelea kuhujumu rasili mali za taifa na badala ya kunufaisha wananchi huwalinda na kuacha mianya ya kujichotea rasilimali za taifa kirahisi bila kuthibitiwa na sharia dhaifu walizozipitisha kwa hila.

    Hii ndio Afrika na siasa chafu za Afrika. Tunahitaji maono na maamuzi mazuri ya namna ya kutumia haki ya kila mmoja wetu kupiga kura ili kuondoa mifumo inayoendekeza hujuma na uchafu unaoendelea kulitesa bara letu zuri la Afrika lenye kila aina ya rasilimali na kutufanya waAfrika wengi kuzalisha malighafi kwa ajili ya kulisha viwanda vya mabeberu huko Ulaya /marekani na nchi tajiri za bara la ASIA.

    Mungu tupe viongozi wenye fikra njema , Wazalendo na watakuwa tayari kupambana na kuhakikisha siku za neema kwa watanzania kwa kuanza taratibu kujenga mifumo ya kuandaa masko ya ndani ya bidhaa za mazao ya kilimo ambayo kwa sasa ni hazina kubwa inayotumiwa na mataifa ya mabara niliyokwisha kuyataja kuendelea kujenga uchumi wa nchi zao na Afrika kubaki katika uzalishaji wa hali ya chini na kukosa fursa za kibiashara na uchumi endelevu kwa sasa na vizasi vijavyo.


    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad