Mfanyakazi wa Radio Clouds Mbaroni kwa Utapeli wa Viwanja.....

Aliyekuwa mfanyakazi wa Clouds Media, Cynthia Maximillan, amejikuta akitiwa mbaroni kwa madai ya kutapeli mamilioni ya shilingi ya wafanyakazi wenzake na marafiki aliosoma nao.
Inadaiwa kuwa mrembo huyo alitiwa rumande kituo cha polisi Oysterbay, baada ya kuwakusanya marafiki zake na kuwapa mchongo kuwa, kuna viwanja vinapatikana huko Bagamoyo kwa shilingi mil 1.5 kupitia Chama cha Mazingira Fukayosi.

Inasemekana kuwa baada ya kupewa fedha hizo mrembo huyo alianza kuwaletea habari ambazo walikuwa hawazielewi na ndipo wakachukua uamuzi wa kumshtaki kwa utapeli wake.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Clouds, Ruge Mutahaba, amedai kuwa anaomba umma ujue kuwa mrembo huyo sio mfanyakazi tena wa kampuni hiyo kwani aliachishwa kazi na yeye pia ni mhanga wa utapeli huo.


CHANZO : MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII/JAMII FORUMS
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu dada namfahamu nilisoma nae ni majanga ana mambo mengi ya ajabu ajabu!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad