Mke: Asha Buheti wa Bongo Movies Amezaa na Mume Wangu wa Ndoa

Gladness Mallya na Gabriel Ng’osha
MAJANGA! Mwanamke aliyejitambulisha kuwa ni mke wa ndoa wa jamaa aliyemtaja kwa jina la Ally Msangi, Rosita Yashira ameibuka na madai mazito kuwa staa wa filamu za Kibongo, Aisha Bui eti amezaa na mumewe huyo.

Akizungumza kwa njia ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp akiwa nchini Peru barani Asia, mwanamke huyo alisema kwamba Aisha amemwibia mumewe huyo ambaye amemtelekeza na watoto wawili na hatoi matumizi.

Alidai kwamba, alifunga ndoa na Msangi, mwenye uraia wa nchi mbili, Tanzania na Peru, mwaka 2007 ambapo wamejaliwa watoto wawili lakini mumewe alibadilika na kuwa na uhusiano na Aisha hadi akaamua kuhamia Tanzania na kuzaa naye.

“Mbaya zaidi Aisha amekuwa akinitumia picha akiwa na mume wangu, akinidhihaki kwamba niwaache wale bata.
“Inauma sana kwa sababu ni miezi saba sasa mume wangu hajui tunaishije na watoto na uwezo anao lakini hatumi matumizi yoyote, ukweli nateseka mno, kwa sasa mtoto mmoja anaumwa, sina fedha za kumtibu.

“Nchi yangu iko kwenye hatari kila siku milio ya bunduki inasikika, hatuwezi kwenda nje kutafuta mahitaji na hata watoto wanacheza ndani, Aisha kaniharibia maisha,” alisema mwanamke huyo.

AISHA ANASEMAJE?
Ili kupata mzani wa habari hiyo, mapaparazi wetu walimtafuta Aisha na kumsomea mashitaka hayo ambapo alisema:
“Ninachojua huyo alikuwa mke wa Msangi lakini wameshaachana na watoto anawahudumia kama kawaida lakini zaidi muulize mhusika baba Paloma (baba mtoto wake, Msangi)  mwenyewe atakueleza ukweli ila najua mapenzi ni kama kiti cha daladala, ukisimama mwenzio anakaa.”

MWANAUME AFUNGUKA
“Hizo habari siyo za kweli, huyo mwanamke alikuwa mke wangu kweli lakini mwenyewe ndiye aliyezingua tukaachana na hivi sasa anashughulikia talaka lakini huwa namtumia fedha za matumizi, hata wiki hii nimeongea naye na nimemtumia fedha.

“Aisha nimekuwa naye baada ya yeye kunizingua kuhusu kumtumia picha za kumdhihaki hilo suala siyo la kweli kabisa,” alisema Msangi.
GPL

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad