Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu akizungumza na waandishi wa habari leo katika kituo cha Stakishari Ukonga jijini Dar es Salaam, kutokana na Askari wa Jeshi la Polisi na raia wa eneo hilo kuuwawa na majambazi waliovamia katika kituo hicho usiku wa kuamkia leo.
Viongozi wa Jeshi la Polisi nchini wakiongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu, wakitembelea maeneo mbalimbali ambayo majambazi walidhuru, katika kituo cha Stakishari Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
*****
ASKARI wa nne wa Jeshi la Polisi na raia watatu wamefariki dunia katika tukio la ujambazi lililotokea katika kituo cha Polisi cha Stakishari kilichopo Ukonga jijini Dar es Salaam.
Katika tukio hilo watu wapatao nane wamesadikika kuingia katika kituo hicho cha Polisi eneo la Stakishari majira ya saa 4 usiku wa kuamkia leo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu amesema lengo la la watu hao ni kutaka kuiba silaha zilizokuwa katika kituo hicho cha Stakishari.
Aidha, amesema wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zinazohusu uharifu kwa Jeshi la Polisi.
Pia, kuhusu uvamizi wa Majambazi, Mangu amesema watajitahidi kuanza kuimarisha ulinzi kwa upande wao hususani katika vituo vya Polisi ndiyo baadae kwenda kuimarisha usalama wa wananchi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Azungumzia Tukio La Majambazi Kuvamia Kituo Cha Polisi Jana.......Asema Waliouawa ni Polisi 4 na Wananchi 3
0
July 14, 2015
Tags