- “Nilitegemea ningefaulu lakini siyo kwa kiwango hicho… hii ni ‘surprise’ (shtukizo),” alisema Gembe alipohojiwa na Mwananchi baada ya matokeo ya kidato cha sita kutangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa.
- “Nawashukuru wazazi, walimu, ndugu na wanafunzi wenzangu kwa kunipa ushirikiano.Nilikuwa nafanya sana ibada hivyo haya matokeo ni juhudi binafsi na majibu ya Mungu,” alisema Ramadhani aliyesoma mchepuo wa fizikia, kemia na baiolojia (PCB).
Historia ya Ramadhani darasani si haba kwani mwaka 2008 alikuwa ni mwanafunzi pekee aliyejiunga na shule ya vipaji maalumu ya Ilboru, Arusha akitokea shule ya Msingi Mombo na alipata daraja la kwanza akiwa na pointi 11 katika matokeo ya kidato cha nne.
- “Siku zote kilichonifanya niongeze juhudi katika masomo yangu ni malengo ya baadaye... mimi nataka kuwa daktari wa binadamu hivyo sikutaka kulegalega kusoma.Pia, wazazi wangu pamoja na hali ngumu walijitahidi kunisaidia kimawazo, kirasilimali na kimaadili…naomba na wazazi wengine wawafanyie hivyo watoto wao,” alisema.
Baba Nurdin Gembe, ambaye ni mzazi wa Ramadhani, alisema familia imepokea kwa furaha matokeo hayo na kwamba alikuwa akiyategemea kuwa mazuri kutokana historia ya kijana wake katika madarasa ya nyuma.“Huyu mtoto namlea kawaida japo zamani alikuwa mtundu sana… ilibidi nimpe mafundisho mengi sana ya kidini bila kupoteza ratiba ya kusoma shuleni.Nashukuru kuwa alizingatia na amefika hapo alipofika,”alieleza Gembe ambaye ni bwana shamba kitaaluma.
This is the news went want to see, in order to promote kids wapende maendelea, Congratuation broth elimu ni kila kitu.
ReplyDeletecograte, hata siku ukiwa unahitaji msaada kwa ajilie ya education weka namba watu watakuchangie. elimu yatanzani emaenda chini sana we need to promote watoto waende shule wasione kuart na kukataviuno ndio maendeleo.
ReplyDeletecograte, hata siku ukiwa unahitaji msaada kwa ajilie ya education weka namba watu watakuchangie. elimu yatanzani emaenda chini sana we need to promote watoto waende shule wasione kuart na kukataviuno ndio maendeleo.
ReplyDelete