Mwanaume Aliyezaa na SHILOLE Ajitokeza na Kudai Hakuwa Kumbaka Shilole Kama Habari zilivyoenea, Adai Shilole ni Muongo

Baba wa mtoto aliyezaa na Shilole amejitokeza na kulalamika kusingiziwa na msanii huyo kuhusu kumbaka..na kusisitiza alikua na uhusiano naye na amekana kumbaka.

Shilole amezungumza na Soudy Brown na kusema mwanaume huyo hajui mtoto anakula nini wala ana miaka mingapi hivyo hataki hata kumsikia kwa kuwa hilo jambo bado linamuumiza na hataki mtoto wake ajue nini kinaendelea kati yake na baba wa mtoto wake.

Pia amesema amepanga kutoa elimu kwa wanawake na wasichana ambao hufanyiwa vitendo vya unyanyasaji kutoka kwa wanaume zao.

Msikilize hapa mtu wangu…


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad