Kulikuwa na stori ya uzushi mitandaoni na June 24 nikamfata nyumbani kwao Sinza na kwenye majibu yake kulikuwa na hiki ambacho nilimnukuu pia >>>> ‘Sio mara ya kwanza kuzushiwa kifo, nasikia mara watu oooh banza kafa, mara ooh kila mtu anaongea lake ila mimi niko poa ni mzima… naweza kufanya kazi ila kwa sasa siko tayari kufanya kazi kwani nitauchosha mwili wangu’
Marehemu Banza Stone
Hiyo haikuwa mara ya kwanza Banza Stone kuzushiwa kifo.. muda mfupi baadae ikaja taarifa nyingine kwamba mwimbaji huyo ambaye alikuwa ni legend wa Muziki wa dansi Tanzania amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala Dar baada ya hali yake kuwa mbaya.
Leo imetufikia nyingine, ni majonzi kwa kila mtu iliyemfikia taarifa hii, Banza Stoneamefariki na hizi ni picha kutoka msibani, nyumbani kwa akina Banza Stone maeneo ya Sinza Kijiweni Dar es Salaam
Mkurugenzi wa African Stars, Asha Baraka akiwa msibani. Banza aliwahi kuwa mwimbaji wa Bendi hiyo kwa kipindi kirefu sana.
kapumzike kwa amani jembe
ReplyDelete