Profesa Anna Tibaijuka Azomewa Tena Kwa Mara ya Pili Jimboni Mwake.......

Aliyekuwa Mbunge wa Muleba Kusini, Prof Anna Tibaijuka anayewania jimbo hilo kwa mara ya pili, jana alishushwa jukwaani kwa kuzomewa na wananchi wake katika kata ya Nshamba wilayani Muleba. Prof Tibaijuka alishushwa jana wakati wa kampeni za kura za maoni kupitia CCM. Hali ya kuzomewa ilidumu kwa dakika kadhaa jambo lililofanya Wagombea hao kulazimika kuondoka. Kwa mara ya kwanza alizomewa juni 8, wakati wa ziara ya katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana katika kata hiyo hiyo. Akiwa na Kinana wananchi walimtuhumu ufisadi wa fedha za Escrow na kushindwa kutekeleza ahadi ya kuwajengea barabara ya lami.
Source: Mwananchi
Nini maoni yako kuhusu hilo?

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ulisema hunanjaa. Na unamapesa ya un Na hata ukazalilisha pesa yetu milion kumi Ni ya mboga. Hufai hata mm naungana Na wanaokuzomea.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad