Rais OBAMA Kumbe Naye Yumo..Hapa Nimekuwekea Video Fupi Akicheza Mayenu Wimbo wa Sauti Sol ya Kenya

Sauti Sol ni kundi maarufu la muziki kutokea nchini Kenya ambalo limefanikiwa kuvuka hata mipaka na kuteka kwenye nchi jirani kama Tanzania, Rwanda, Burundi na nchi nyingine za Afrika mpaka kupelekea kuwa nominated kwenye tuzo kubwa kama za MTV na BET 2015.

Kundi hili lilipata mwaliko maalum wa kwenda kuimba Ikulu ya Kenya kwenye party ya kumkaribisha Rais Barack Obama wa Marekani ambaye baba yake mzazi ni mzaliwa wa Kenya.

Tazama kwenye hii video fupi hapa chini jinsi Sauti Sol walivyokuwa wakiperfom na baadae Rais Obama na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kuungana nao kucheza.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. A fresh breath of air! So nice. Life is good jamani penye upend. .. haijalishi wewe Rais au kuli.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad