Snura Ampiga Vijembe Wema Sepetu

Aliyewahi kuwa swahiba  wa mbunge  mtarajiwa  Wema Sepetu, Snura Mushi ametoa kauli zenye mlengo  wa kumpiga vijembe Wema.

“ Naepukana na unafiki  tena naweza kusema ni  roho mbaya chuki kwa baadhi ya wasanii kuunda makundi ambayo yanatumia muda  mwingi  kuwadis wengine, mfano hivi sasa wakata Diamond anawania  tuzo za kimataifa  eti kuna watu wanaungana na watu wan je kufanya kampeni ashindwe,” alisema Snura.

Snura anadai kuwa  siku hizi makundi  ambayo  yanaundwa na wasanii au wapenzi wenyewe ambayo yanatumika vibaya  katika kutengeneza ugomvi au kushabikia wasanii wakigombana kwa kutumia mitandao ya kijamii kuwatusi na kuwakatisha tamaa hata kama wanafanya kazi zinazotangaza Taifa.

Wema Sepetu ni miongozni mwawasanii ambao wanadaiwa kuhamasisha kundi lake “team Wema” kumpigia chepuo msanii wa Nigeria Davido ambaye anachuana na Diamond wa hapa nyumbani katika tuzo za MTV Africa MAMA.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wivu tu na roho ya kwa nini..........

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad