Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa alitambulishwa rasmi kuhamia CHADEMA July 28 2015 Dar es Salaam akiwa ameongozana na mke wake, Regina Lowassa pamoja na watoto wao.
Kwenye list ya Viongozi wa UKAWA ambao walikuwepo kumpokea na kumkabidhi kadi ya CHADEMA, alikuwepo James Mbatia, Prof. Lipumba, Dk. Emmanuel Makaidi, Salum Mwalimu na Freeman Mbowe.
Salum Mwalimu ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, amesema haya kuhusu mapokezi hayo >>> ‘Tunashukuru sana Watanzania, sidhani kama kuna kiongozi wa CHADEMA simu yake iliwahi kuzidiwa kama jana, simu zilizidiwa kwa pongezi… Kila mtu amezungumza kwa sababu ya Historia ya tendo lenyewe‘>>>>
‘Kesho Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa atachukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA… pengine kutakuwa na shamrashamra nyingi itategemeana na Mgombea mwenyewe, akiamua kuja na mdundiko haya… lakini tunaamini kutakuwa na shamrashamra nyingi‘ >>>> Salum Mwalimu.
Stori zikaanza kuzushwa kuhusu sababu ya Viongozi wengine wa UKAWA kutokuwepo, majibu kayatoa pia Salum Mwalimu>>> ‘Tuna mambo mengi tuna mikakati mingi, tumegawanyika… sio kila tukio wote tuwe pamoja, jana mliuliza Tundu Lissu yuko wapi na leo huyu hapa hata hamumuulizi… Tuko kwenye kipindi cha Uchaguzi tuna mambo mengi hatuwezi wote kuwa sehemu moja, tunagawanyika kutokana na ratiba tuliyonayo
Tundu Lissu, Dk. Slaa hawakuwepo Lowassa alivyopokelewa CHADEMA.. Sababu ni hii hapa (Audio)
0
July 29, 2015
Tags