Unamfahamu Dadake Rais Obama,Auma Obama?

Msemo wa kuwa damu ni nzito kuliko maji ulidhirika wazi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi Kenya ijumaa usiku.
Hiyo ni baada ya rais wa Marekani Barack Obama kuweka historia kwa kuwa kiongozi wa kwanza wa taifa lenye nguvu zaidi duniani kukanyaga ardhi ya Kenya, picha zilizosambaa kote duniani zilikuwa za rais Obama akimkumbatia mwanamke aliyekuwa mwisho kabisa katika foleni ya wale waliomkaribisha nchini wakiongozwa na mwenyeji wake rais Uhuru Kenyatta.
Je Uliiona picha hiyo ?

Mwanamke aliyepigwa picha akimpiga pambaja rais Obama na hata wakaondoka naye katika gari lake maalum al maarufu ''The Beast'' si mwengine bali ni dadake wa kambo Daktari Auma Obama.
Rais Obama alimbusu bi Auma Obama na hata akazungumza naye kwa muda mrefu huku rais Uhuru Kenyatta akimsubiri.
Zaidi ya hayo, Auma aliruhusiwa na maafisa wa usalama kutoka Marekani kuingia ndani ya ''The Beast''.
Wakenya wengi na watu wengi waliachwa vinywa wazi wasimjue ni nani.

Auma humsifu nduguye ambaye humuita '' Barry''
Aidha ukuruba wake na rais Obama uliibua hisia mseto huku kila mmoja akitaka kujua zaidi kumhusu Auma Obama.
Auma Obama au Dakta Auma jinsi anavyofahamika zaidi, ana mwenye umri wa miaka 55,alipata umaarufu zaidi baada ya Rais Obama kumnukuu kwenye kitabu chake cha 'dreams of my father' kwa kuwa dadake wa kambo.
Baada ya kifo cha baba yao Senior Obama mwaka wa 1982, kila mmoja wao alianza safari ya kumtafuta nduguye.

Licha ya ndugu hao kulelewa katika mataifa tofauti na hata kutengana kwa muda mrefu, mwishowe walikutana mnamo mwaka wa 1984 kufuatia ualishi wa rais Obama. Walikutana jijini Chicago, Marekani.

Miaka 28 iliyopita wakati Rais Obama aliwasili nchini Kenya, Auma alienda kumpokea katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kwa gari la muundo wa Volkswagen.
Gari ambalo rais Obama mwenyewe alileza kuwa lilikuwa gari kuu kuu.
Auma humsifu nduguye ambaye humuita '' Barry'', kwa kuinua hadhi ya familia ya babayao.

Auma aliruhusiwa na maafisa wa usalama kutoka Marekani kuingia ndani ya ''The Beast''.
Auma alikuwa katika harusi ya Obama mnamo mwaka wa 1992 kama masaidizi wa Michelle Obama.
Auma anaendesha wakfu wa kuwashughulikia mayatima unaofahamika kama Sauti Kuu.
Kulinagana na Auma, kituo hicho, hutumika kuwakuza watoto mayatima na wengi wao wanaendelea na masomo.
Aidha amesomea nchini Ujerumani na kuishi Uingereza kwa muda mrefu.

Auma hushinda kwa kipindi kirefu akiwa na bibi yao, Bi Sarah Obama
Auma amesomea masuala ya sanaa na anapenda kuwasaidia watu wasiojiweza katika jamii.
Dkt Auma alilieza jarida la TIMES kuwa yeye anapenda maisha ya kawaida.
Licha ya kuwa na uhusiano na rais mwenye ushawishi mkubwa zaidi duniani, anapenda kuendesha shughuli zake za kibinafsi.
Auma hushinda kwa kipindi kirefu akiwa na bibi yao, Bi Sarah Obama katika kitongoji cha Nyangoma, Kogello ambapo babake Rais Obama Sr obama alizaliwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad