Baba na mama wa mke wangu walikuja mwaka 2011 kututembelea hapa Dar, ilikua wakae mwezi mmoja then warudi kijijini
lakini cha kushangaza hivi ninavyozungumza nanyi tarehe 30-06-2015 jumanne, hawajaondoka kurudi kijijini kwao hadi Leo miaka takribani minne tangu 2011 January
Kijijini kwao si kubaya kihivyo, kuna nyumba ya bati, kulikua na mifugo na mashamba lakini vyote hivyo vilikufa kutokana na kutelekezwa na mwenyewe ambao wamekimbilia kwetu Dar. Ni nyumba tu ndo ipo pale ila imekua pagala.Ndugu wengine wapo mjini ila mikoa tofauti.
Madhara yatokanayo na wakwe kukaa kwetu:-
(1) Kila tukigombana namke wangu au kutofautiana hata kwa jambo dogo sana, kesho yake atawaeleza wazazi wake, jioni yake wataniita kulizungumza, hadi nakereka, kila siku nawekwa chini hata kwa Yale ambayo zamani tulimaliza chumbani
(2) Kwa muda waliokwisha kaa baba mkwe amefanya nyumba yangu kama kwake, anatoa amri kana kwamba yeye ndo mwenye mji, anawa amrisha familia yangu chakula cha kupika ambacho ni kinyume na nitakavyo mm, na taratibu zingine za kikoloni
(3) Kabla hawajaja 2011, tulikua na Chumba special cha wageni wetu maalum self contained, ambacho sasa tumewapa wao hivyo wageni wetu tunawalaza kwa watoto, watoto tunawahamishia kwa house girl, kama wageni ni wengi house girl hulala sebuleni, jambao ambalo huwa linaniudhi sana sana
(4) Gharama za maisha zimekua kubwa, kuishi kwao, afya zao, mahitaji yao ni juu yangu, ukijumlisha na familia yetu mzigo unakua mkubwa sana
Wakuu, kwa hali hii nimeshindwa kuendelea hivi najitaji way out, niliamua kukaa na wife tuweze kujadiliana kuhusu wazazi kurudi kijijini lakini kinyume na matarajio yangu uligeuka ugomvi mkubwa sana, akasema kama siwataki wazazi wake niseme wazi badala ya kujifanya namshauri,
Tangu siku hiyo ni visa tupu, kadai kwamba wazazi wake hawaendi kokote, kama nimemchoka anadai nimwambie aondoke yeye na wazazi wake, baada ya kuona diplomacy imeshindikana ikanibidi niwe mkali, ingawa sikufika hatua ya kumtamkia kwamba nawafukuza wazazi wake
Nimekua nikimuuliza "" hivi kule kijijini wazee wako walifanya kosa gani hadi kufikia hatua hawataki tena kurudi pamoja na misaada yote tuliokua tukiwatumia? Anakaa kimya
Mbona mimi wazazi wangu wapo kijijini wanaishi vizuri tu na wanayapenda maisha ya kule? Na tunawatumia misaada na wameridhika?
Ingawa sote mimi na wife tunafanya kazi ila kama mwanaume mimi ndo nabeba karibu robo tatu ya gharama za uendeshaji familia i .e ada za watoto na bill mbali mbali na kadhalika
Juzi nimekutana na a primary school friend, tulipotezana miaka mingi sana, she was so bright in school, she is successful, anafanya kazi katika health sector, tulikutana katika function flan tukabadilishana business cards, tumetoka out kwa maongezi ya kawaida kama mara tano hivi, tumekumbushana vitu vingi sana vya enzi hizo, tuli enjoy sana kuongea pamoja
Hivi karibuni alini invite kwa ajili ya lunch Jumamosi moja nyumba ni kwake, aliniuliza napenda nn nikamwambia Biriani,
So akaniambia niende kwake ameaandaa Biriani.Tulikula pamoja, na tuka watch movie, although hakuna kibaya kilichotokea kati yetu ila nilimueleza matatizo yaliyopo Kwangu, akaniambia kama vipi tunaweza kuwa pamoja ila nichague sehemu moja yeye hawezi ku share.
Anyway, sijajua kwa nn hajaolewa hadi Leo ingawa yupo kwenye mid 30s . Ila aliniambia kwamba kwenye health sector shule inachukua Muda mrefu kumaliza kuliko sector zingine ukichukulia kwamba alifanya na masters pia.Waheshimiwa kwa kweli nilikua suffocated kwa Muda mrefu nyumbani kwangu walau sasa nimepumua kidogo
Nalileta hili tatizo mikononi mwenu kwa ufumbuzi zaidi, mke wangu nampenda ila kwa sasa hatuelewani kabisa, chanzo ikiwa ni wazee wake ingawa na mengine mengi yameingia hapo hapo
Nilimuomba rafiki yake kipenzi azungumze nae kiutu uzima amweleweshe kuhusu wazazi kutuachia nafasi ya kupumua lakini hivi navyozungumza nanyi urafiki ulikufa, aliambiwa anathubutu vipi kuingilia ndoa yetu! Ukawa ndio mwisho Wa urafiki wao, na hadi sasa naambiwa natembea nae wakati si kweli
Au nikubali pendekezo la moreen? Mengine yatajijua huko mbele?
Peleka watoto bording, mrudishe housegirl home kwao then tafuta kazi mkoa mwingine au omba uamisho wa muda, kwa sababu hajazoea kuudumia familia lazima atatafuta cha kufanya kwa mwezi tuma pesa kidogo ya kufika katikati ya mwezi au usitume kabisa.
ReplyDeleteHata maandiko matakatifu hayapendi hivyo.
DeleteVipi wangekuwa wazazi wako?
ReplyDeleteKwa Moreen kaka panafaa.
ReplyDelete