Wazazi wa Mwigizaji ROSE NDAUKA Wacharuka....Hawamwelewi Mtoto Wao Kuhusu Wanaume..Wampa Onyo

Staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka hivi karibuni amewekwa chini na familia yake na kupewa onyo kuhusu wanaume pamoja na maadili.

Kwa mujibu wa chanzo, Rose aliambiwa maneno mengi na familia yake ikimtaka ajirekebishe na haswa ajitume zaidi katika kazi zake anazofanya.

“Familia yake imeamua kumuweka chini na kumwambia mengi kuhusu maisha haswa ikimtaka ajirekebishe tabia yake kwa ujumla,” kilisema chanzo.

Rose alipotafutwa kuweka wazi juu ya hili, alifunguka;
“Kila familia ina utaratibu wake, kwahiyo mimi kuwekwa na familia na kupewa onyo wala siyo suala la ajabu.”

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dada litunze hilo ua sasa umpate mwenzako atakayeweza kukusaidia kulitunza fresh ili liendelee kung'aa ukingojea mpaka lisinyae jasho litakutoka dadaangu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad