Alikiba Athibitisha Ujio wa Collabo yake na Davido, Aelezea Ngoma itakuwaje

Habari kuhusu ujio wa collabo kati ya superstar wa Nigeria, Davido na superstar wa Tanzania Alikiba tuliisikia kutoka kwa Davido mwenyewe wakati wa tuzo za 2015 MTV MAMA zilizotolewa huko Durban, Afrika Kusini.

Hatimaye Alikiba naye amezungumzia collabo hiyo kwa mara ya kwanza, kwa kuthibitisha kuwa alichokisema Davido ni kweli hivyo watu wajiandae kupokea kazi hiyo hivi karibuni.

“Davido ameongea na Millardayo kwamba anataka kuja kufanya featuring na Alikiba, which is tayari tulikuwa tumeshaongea muda mrefu, kwahiyo watu wasubirie tu ngoma inakuja kutoka lini.” Alisema King Kiba kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm.

Alikiba pia ameelezea kile ambacho wanatarajia kukiimba katika wimbo huo ambao bado haujarekodiwa.

“Track iko vizuri, lakini idea bado haijakamilika, lakini kiukweli mi hua nafanya ngoma nikiwa studio, tutazungumzia kuhusu goodtime, party, mapenzi flani you know, yaani nyimbo flani ya kuhamaishisha watu katika raha.”

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. BORA TUPATE SUPER STAR WA PILI MKUBWA TOKA TANZANIA.. nina Iman na Alikiba hanaga uchoyo wa kuwainua watanzania wenzake..
    NAJUA atafanya na ataweza na ATAINUA WENGI SANA
    ..

    ReplyDelete
  2. Huna jipyaa kama ulifanya na Rkely bado haikusaidiakitu itakuwa kwa msanii mdogo kama davido

    ReplyDelete
  3. Kaza buti Ali utafanikiwa tu, hata ukianguka mara saba bado nyanyua mzigo wako endelea mbele yalipo mafanikio yako, utafika tuu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad