Michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na kati Kagame Cup 2015 imemalizika August 2 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa kupigwa michezo miwili wa mshindi wa tatu na mchezo wa fainali.
Mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ulipigwa kuanzia saa 7:30 mchana kwa kuzikutanisha timu za KCCA ya Uganda dhidi ya Al Khartoum ya Sudan, mchezo ambao umemalizika kwa KCCA kushinda kwa jumla ya goli 2-1.
Baada ya hapo ulipigwa mchezo wa fainali uliozikutanisha timu za Azam FC kutokea Tanzania na Gor Mahia kutokea Kenya huo ni mchezo wa sita kwa Azam FC kucheza bila kufungwa katika michuano ya Kagame.
Azam FC imeifunga Gor Mahia ya Kenya goli 2-0 huku magoli ya Azam FC yakifungwa na nahodha wa timu hiyo John Bocco dakika ya 16 kipindi cha kwanza huku goli la pili likifungwa na Kipre Tchetche dakika 65, kwa matokeo hayo Azam FC ni bingwa wa Kagame Cup 2015.