Bongo Star Search ni Janga la kitaifa...Mchakato Umejaa Dharau, Kejeli na Kukatishana Tamaa

Kwa mtu yeyote intellectual ambaye huwa anatazama Bongo Star Search atakubaliana nami kuwa mchakato huo wa kusaka mwanamuziki bora mwenye kipaji umejaa dharau,kejeli na kukatisha tamaa,hawa Master Jay na Salama Jabir ni majaji feki kabisa wanaowakatisha tamaa vijana wenye vipaji,namsifu sana Madam Rita, dada huyu hajawahi kumkatisha tamaa mshiriki yoyote,hata anapoonekana kushindwa yeye humtia moyo ama kukaa kimya,lakini salama na master jay huwatolea maneno ya kejeli,vijana wangu wa Tanzania wenye vipaji mbalimbali msikatishwe tamaa na hizi taasisi za kihuni zinazojifanya zina uwezo wa kubaini vipaji vyenu,leo hii Diamond, Lady Jay Dee, Prof Jay, Dully sykes na wengineo wangeenda kutafuta vipaji vyao Bongo Star Search wangerudi wakiwa wamekata tamaa kwa kukutana na kina Master jay na Salama, simameni wenyewe achaneni na hawa wahuni, mtapoteza vipaji vyenu bure, historia inaonyesha kuwa, hakuna mtu aliyefanikiwa maishani kwa kuwekwa katika mizani ya ushindani bali alifanikiwa kwa kujituma mwenyewe akiamini atafanikiwa

By  Dilemma.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ila sawa, lakini hata kama ni wewe ndiye jaji ungekubali vijana wanaokuja na nyoka na vyura ndani ya ukumbi au katika stage? hapo hapo kundi la vijana ni wengi mno, wapo nje wanasubiri kuonyesha vipaji?. samahani sana kama umetolewa na uje uongee katika media ! wewe umewahi kufikiri wenye kuandaa programu hiyo na wadhamini wanatoa ela wapi?. mtu anaenda kuonyesha kipaji lakini anafika anaanza kumbusu salama aidha hewani au anamfuata kabisa! ni ujinga. Watanzania wajitayarishe, waimbe vyema kama yule Alfa wa Rwanda katika Tusker ile na kina Msechu (mtz). c uchuro! la sivyo tunacheka sana bana..... maana wengi ni "makomedian'' kumzidi hata joti, masanja mkandamizaji nk, ndo maana salama huwakatisha tamaa ili wajaribu kuona fursa zingine maana wengine hawajui kabisa kuimba, wala hawajajitayarisha.

    ReplyDelete
  2. Na hata hao wanaopewa maneno mbofumbofu wanamoyo, kama mimi ningewasubiri nje mmoja mmoja nikawakata kidafu!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad