CCM Wayapuuza MAFURIKO ya Lowassa......Nape Asema Hata Mrema Alikuwa Kivutio. Ataka Gari la WAGONJWA Lipelekwe Kwa Lowassa Mapema

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesisitiza kuwa kitashinda Uchaguzi Mkuu mwaka huu kwa sababu kina mtandao mkubwa wa wanachama kuanzia ngazi ya chini na kwamba kufurika kwa wananchi katika mikutano ya Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa sio ushindi, kikisema kura ni mahesabu.

Aidha, kimesema kuwa mgombea huyo wa Chadema na umoja wa vyama vinne vya upinzani (Ukawa), amedanganywa na wapambe wake kuihama CCM na kumkejeli ikisema gari la wagonjwa linapaswa kuwekwa nyumbani kwake siku ya uchaguzi kwani CCM itapata ushindi wa uhakika asubuhi.

Akitoa taarifa kuhusu kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika jana katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisisitiza kuwa ushindi wa chama hicho tawala na kikongwe hauna shaka kutokana na mtandao wake kuanzia ngazi ya chini.

Akijibu swali kuhusu kufurika kwa wananchi katika mikutano ya mgombea huyo wa Chadema, Nape alisema:

“Kwa walioanza siasa jana ndio watashituka. Mwaka 2010 Slaa (Dk Willibrod) katika mkutano wake wa mwisho wa kampeni Mbeya alipata watu wengi kuliko wale aliopata Edward. Lakini kura alizopata Mbeya utashangaa.

“Kupata watu wengi mkutanoni hakutushangazi kwani kura ni mahesabu, hawa (Chadema na mgombea wao) wanatoka pointi moja kwenda nyingine. CCM ina mtandao, ukiondoka mjumbe wa nyumba kumi anapitia watu wake anasafisha nyayo zenu,” alisema kiongozi huyo.

Nape aliongeza kuwa wapinzani wote wametoka ndani ya CCM kuanzia kwa Augustino Mrema mwaka 1995 na hadi katika chaguzi nyingine zilizofuta na zote wapinzani walishindwa, na hata safari hii CCM itashinda.

Akimgeukia Lowassa, Nape alisema Waziri Mkuu huyo aliyejiuzulu, amedanganywa na wapambe wake na kuondoka chama tawala, na kwamba licha ya kuhamia huko, CCM itamshinda asubuhi na kuwataka wanaotishia kukihama kufanya hivyo na si kuleta shinikizo.

“Katika mchakato wa uchaguzi si wote watakaoridhika na matokeo kwa sababu kuna wengi wanajiandaa kushinda na sio kushindwa, na matokeo yanapokuwa hivyo, wanakuwa hawaridhiki na hapo ndipo wanazungumzia kwenda upande wa pili, na hasa kwa shinikizo la wapambe.

“Hili limetokea kwa Edward, amekwenda upande wa pili, amedanganywa na watu, tutampiga. Ushindi wa CCM ni wa uhakika, sio wa matumaini. Matumaini yapo Angaza, CCM ni ya uhakika. Tutashinda asubuhi. Tumesema ni mpambano kati ya wagombea na makapi,” alisema Nape na kuongeza:

“Zipo mechi ambazo unajua hii utashinda. Yanga na Lipuli ya Iringa unajua matokeo yake. Tunataka mgombea mwenzetu apelekewe ambulance (gari la wagonjwa) nyumbani kwake, kwani ushindi kwetu ni uhakika.

” Kuhusu wanaolalamika na kutishia kuhama, alisema malalamiko hayawezi kutolewa barabarani kwani chama hicho kina utaratibu wake na yale yote yaliyolalamikiwa yakiwamo ya udiwani, yamefanyiwa kazi.

 “Tulisema wakati ule wa mchakato wa kutafuta mgombea wa urais kuwa hatutafanya kazi kwa shinikizo. Tunajua uimara wa chama chetu, kama kuna watu wanataka kwenda upande wa pili waende. Lakini CCM haiwezi kufanya kazi kwa vitisho na shinikizo.

"Tatizo ni kwamba kunatokea wagombea 12, halafu unasema lazima uwe wewe. Kuna watu (wanaotaka kuhama) wanafanya hivyo kwa shinikizo la viroba na hela,” alisema Nape.

Post a Comment

16 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ushindi hauna shaka si kwa kuiba kura?nani asiyejua mliiba kura last election?na wewe nape ulisema ata kwa bao la mkono?ndio mtandao mkubwa huo lakini safari hii imekula kwenu tutalala kulinda kura ipasavyo tanzania nzima hatubanduki mbwa kala mbwa.

    ReplyDelete
  2. Subiri uone nape trust me utatafuta kwa kujificha,hivi nape hizo gurds za kulopoka hivyo unazitoa wapi?hata Kama unatumwa unashindwa kuchanganya Na za kwako!

    ReplyDelete
  3. We mchangiaji hapo juu,unasema nape achanganye na zake kwann na kwann awe mnafki wacha aseme anachojisikia mbona ukawa wanasema mengi sana km wazaramo wa msanga hatusemi wakisema ccm kosa,wacha aseme,hajatumwa na wala hatumwi na mtu.
    C Kidumu chama cha Mapinduziiiii ,mtakoma na mizigo yenu mlioamua kuibeba sababu ya hela ikulu mtaiona kwa nje msituletee vurugu tu,maana ukawa kwa kupenda mabomu hamjambo.

    ReplyDelete
  4. ccm mbele kwa mbeleeeee. watawezaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Thubutuuuuuuuu, mziki wa CCM 'ukawa' hawauwezi, watasubiri sana tuuu

      Delete
  5. We mchangiaji hapo juu,unasema nape achanganye na zake kwann na kwann awe mnafki wacha aseme anachojisikia mbona ukawa wanasema mengi sana km wazaramo wa msanga hatusemi wakisema ccm kosa,wacha aseme,hajatumwa na wala hatumwi na mtu.
    C Kidumu chama cha Mapinduziiiii ,mtakoma na mizigo yenu mlioamua kuibeba sababu ya hela ikulu mtaiona kwa nje msituletee vurugu tu,maana ukawa kwa kupenda mabomu hamjambo.

    ReplyDelete
  6. NAPA MATAKO YA MAMA YAKO MTAMA HATUKUPI KURA NYOKO WEWE

    ReplyDelete
  7. Mimi ni Mwanachama Mwanzilishi wa CCM Kadi yangu ni Nambari A226415 Niliyokabidhiwa mnamo tarehe 27 March 1977 Nikitokea TANU.Siku zote Falsafa yangu ni ukweli na upendo.Kwa duru za Kisiasa Zinazoendelea sasa,NAPENDA KUKIRI KWAMBA CCM TUPO KWENYE ANGUKO KUU.VIONGOZI WETU WAANDAMIZI WAKIONGOZWA NA KITI WALIYATAKA WENYEWE.KILIO,KILIO,KILIO.OOOOH MUNGU WANGU

    ReplyDelete
  8. CCM in blood kidumu chama tawala..................penda sana ccm tena baada ya kumteua Magufuli
    Namkubali magufuli adi nasikia haja kubwa..................more love for Magufuli baba yangu bado cku chache tu nitaanza kuitwa jina langu G. M . MAGUFULI

    ReplyDelete
  9. Nape nauye jembe letu kukubali sana kaka..................UKWAWA CJUI ndo mnajiita andaeni gari la wagonjwa october. pole zenu msojielewa nyie a.k.a bendera fuata upepo

    ReplyDelete
  10. ni mgonjwa ,nchi siku zote imeongozwa na viongozi wenye afya ,hatuwezi kukubali kuongozwa na kiongozi unhealthy .hatuna pesa za kuitisha uchaguzi mwingine .hana sifa za kuongoza nchi .mroho wa madaraka ,anataka kwenda kufanya nini ikulu ,anataka kutuletea fujo ,hayuko tayari kushindwa ,mkataeni .nchi hii inakuja kufanyiwa mambo mazuri na dr. pimeni watuhawa wawili kisayansi na siyo kungangania mageuzi lazima.mageuzi yataletwa na dr na siyo huyo babu.hawezi kuongea kwa kusimama hata 30minutes .atatuwakilisha vipi nje? atawezaje kuhutubia mikutano ya kusimama kwa one hour .vijana acheni oyaoya haitowasaidia

    ReplyDelete
  11. C C M wawaaaaaaaaaa,ukawa imekula kwaooo

    ReplyDelete
  12. CCM ni chuma cha reli hakipindishwi kwa goti

    ReplyDelete
  13. Je ikitokea ccm wameshindwa na nyinyi mletewe nini ndege ya kwenda ulaya kucheck bp ama!! kwa nini unawasemea watz kama upo kwenye akili zao bwana!! usitudanganye maana palipo na mzoga ndipo watakapo kusanyika Tai," na tai si unaona mwenyewe wanapokusanyikia! ha, ha, ha, ha, haaaa....

    Halafu wewe unao wasema wazaramo ebu taja kabila lako hapa tulijue ili tupate kulijadili kwanza, yawezekana ndio nyie mliokimbia uchawi kwenu na kuja dar, na hapa mkakutana na majini au vipi!?

    ReplyDelete
  14. Nyie mnao ishabikia ccm wamewafira hao ccm ndio mabwana zenu kumanina zenu

    ReplyDelete
  15. ccm ni chama chenye ukimwi sasa hivi. na bwana Guninita amesema "daktari anaona kwamba mwisho wake umefikia sasa" - tuandae tu sanda na sanduku la kubebea ccm iende kuzimu!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad