Leo nikiwa napita napita kwenye mitandao ya kijamii nikaingia kidogo kwenye huu mtandao wa instagram..
Nimezoea kuona msanii Diamond aliyejitoa akili akimpost Magufuli na kumsifia kwa mambo mengi(hakuna tatizo hapa,ni ujinga wake na ni lazima uheshimiwe)..
Lakini leo nimeshangaa kwa kitu alichoandika,eti waliohama wote ni wakabila moja(Lowasa,Sumaye)..
Sina shaka alichoandika hakijatoka kichwani mwake bali ameagizwa(hilo sote twalijua)..
Tunajua wasanii wote walikua wana msapoti Lowasa mpaka walipoitwa kwenye dinner na kulainishwa na mwanasiasa bora,kuliko wote Tz,Mh.J.kikwete(kumbuka ni mwanasiasa bora na sio kikngozi bora).
Diamond, Ni Nani Kakwambia Sumaye na Lowassa ni Kabila Moja? Hii Sasa Unaleta Ukabila....
16
August 25, 2015
Tags
Kwani mngoni na mndendeule si wote ni walewale tu?
ReplyDeleteMnyasa na mmatengo jeeeeeeee?
Mmakonde na Myao nao utasemaje?Wee mwandishi una lako.Hamnazo!
hapo kakosea nini? wote si wanatoka kilimanjaro?????????? acha ushamba we mwandishi
ReplyDeletewewe nawe hauelewi lolote kaa kimya,wote hao hawatoki kilimanjaro,rudi darasani
DeleteDOGO NAE KAJISHUSHIA HESHIMA KWA WATANZANIA WALIOKUWA WANAKUHESHIMU. HATA KM KUJIPENDEKEZA KWA MSANII MWENZENU BUT THIS IS TOOO MUCH,NAKUFANANISHA SASA NA KADA NAMBA MOJA WA CCM BWANA POLEPOLE
ReplyDeleteTusiwe wajinga wakusoma habari na kutoa maoni bila kutafakari ila jamaa huyo mwandishi kapigika na sisi wasomaji tuwe waelewa tusiwe wapumbavu wa kufagilia swaga za watu wahuni za kuleta uchonganishi hivyo alivyoandika Diamond hakutaja Lowassa wala Sumaye kazungumzia ukabila kwa ujumla usitutenganishe au kuwekewa ukabila nchini wote ni wamoja tupendane sasa tatizo nini maoni mengine ni yakutafuta kicki kuisaidia UKAWA kinyemela na UKAWA haiwezi kujenga sera za kuaminika ila kupitia kwa wahuni wanaopotosha ukweli na hicho kitu kinachofanya jahazi lao kuzidi kuzama kila kukicha na kubaki na miziki ile ile ya kizamani lazima CCM ing'oke huku wanadidimia nakujifanya kama wanahaki ya ndiyo kwa watanzania wote na ndo wawakilishi wa kura zote za watanzania msijidanganye na huu upuuzi uzeni sera za maana sio kuandika matusi na kashifa watu mnawaboa na kuwaona si kitu mali
ReplyDeleteMbulu na mmasai wote ni wavaa mshuka
ReplyDeleteNi yeye Sumaye ndio analeta ukabila aliposema wanataka rais kutoka kaskazini
ReplyDeleteHatakama sio kabila moja lakini wote ni'wakaskazini a.k.a. Arusha, ni wabinafsi mno....lakini mwisho wao unafika labda waunde ufalme wao wa kanda ya kaskazini.....CCM oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
ReplyDeleteNdo mana makabila yanatajwa kwa idadi yake. Mmakonde na myao ni tofauti. Kiukwel shule bado ndogo kwa baadh ya watu.
ReplyDeletedomo linaropoka tu, au linafikiri watu waliotoka kaskazini wote ni kabila moja, kumbe hata Tanzania haijui vizuri eehh!! au elimu ndogo!
ReplyDeleteChadema wote ni waropokaji tu suala la Chama ni sawa na Itikadi za kidini kwani kuwa na mapenzi na ccm dhambi??
ReplyDeletechadema wote wahuni tupu Diamond Perfect kama mna hasira futa nyimbo zake kwenye simu sisi ndiyo tunazijaza
sio vibaya kuonyesha Hisia za mapenzi ya chama
ndiyo maana hata Lowasa kahama CCM akiwa mzee mbona hakutoka akiwa kijana?
imekula kwenu na chadema mwaka huu wa mwisho chama kimekufa
domo akili yake ipo mdomoni,darasa lenyewe la form 2,go back to school.
ReplyDeleteyeye ndo analeta ukabila nani alyezungumzia ukabila?ndo tabu ya kupigiwa kampeni na watu waliosoma tandale
ReplyDeleteDogo piga music wako tu ndugu yangu kujua kiingereza sio eti una akili , najua Huna njaa sasa kwanini unakubali kutumika "kusapoti" majambazi? Uko juu kwanini unataka kujishusha mwenyewe? Hivi kweli sumaye na mbowe ni Kabila Moja? Ccm sio mbaya Bali Watu wameichoka wewe umewatema madem wangapi?
ReplyDeleteUpeo ni Mdogo sana kwa mwandishi na hata diamond upeo wake ni Mdogo mno angekuwa na upeo mkubwa angetumia siasa kama moja ya vyanzo vyake vya mpunga sio kuleta ushabiki ambao mbeleni hautamsaidia kwa lolote
ReplyDeleteHivi kosa la Diamond ni kupenda CCM. Acheni hizo. Kila mtu ana haki ya kuchagua chama anachokipenda. Mnadhani Watanzania wote ni CHADEMA? Mshindwe na mlegee...
ReplyDelete