Gazeti la Uhuru: Vijana waliomsindikiza Lowasa kuchukua fomu jana ni VIBAKA

Ni kitambo sana gazeti dada la chama Cha Mapinduzi limekua likinanga Harakati za vyama pinzani. Yote tisa kumi ni ripoti zilizomo kwa gazeti hili tar 11/08/2015 siku moja baada ya MTETEMO WA UKAWA JIJINI DAR.

"Ati Kundi la vibaka latikisa Ukawa. " hao vibaka mliwaona wapi, hizo fedha walizolipwa mliziona kwa nani, na hizo Pombe walizokunywa mliwanywesha?

Mmeanza kukata mauno hata ngoma bado haijaanza kudunda? Mtachoka mapemaaa. Kama Gazeti ni la kimapinduzi wapeni watu habari zenuu, msiwapotoshe watu kwa vitu walivyovishuhudia.

Niwaulize kidogo.

Hiviii Wizi wa kura katika michakato ya majimboni si habari? Semeni hayo.

Na je Rushwa iliyoota mizizi katika Harakati za uteuzi si habari? Andikeni hiyo.

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Asante hapo umemaliza kila kitu,naona hicho ndo walichoambiwa Dodoma hawana jipya hao siku nyingi na hakuna wakusoma habari zao

    ReplyDelete
  2. kibaka ni yeye aliyeandika hii habari!!

    ReplyDelete
  3. Kama gazeti la UHURU wangekuwa na busara, wangekaa kimya tu kuliko kuongopa

    ReplyDelete
  4. WAANDISHI MTATAJIRIKA SANA MWAKA HUU!MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  5. Nikweli kabisa, wengi wao kutoka buguruni walikuwa 'bwiii', na kweli kuna eneo walipora

    ReplyDelete
  6. waambie hao,watachafua sana lakini aonaye haambiwi tazama!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  7. Umeshasema gazeti la UHURU ,na ata Kama ni vibaka lakini wote walikuwa na shahada ya kupigia kura na watapiga kura siku ya siku sababu wana haki

    ReplyDelete
  8. wafamaji haoooo hawaachi kutapatapa hahaaa........chezea mziki wa ukawa weye .......WATADEKI BAHARIIIII

    ReplyDelete
  9. hao wanao waona vibaka ndio watakawaondoa madarakani, maana wana haha vibaya! wtz tuwe na mshikamano tusiwasikilize hawa.

    ReplyDelete
  10. MMMM WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KAKANUSHA!!! AIBU YENU UHURU!!!! HABARI SIO ZA KWELI.

    ReplyDelete
  11. Nyie gazeti la uhuru, mbona waliomsindikiza magufuli walikuwa wameanza viroba, je hiyo haiku a habari ya kuandika. You journalists at the government owned newspapers are so myopic that we'll start to doubt your professionalism

    ReplyDelete
  12. TAARIFA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI HII HAPA CHINI. UHURU KAA KIMYA!!!

    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe

    “Tunaomba wanasiasa na mashabiki (wafuasi) wao wasitembee na silaha kwenye mikutano yao, waziache mahali salama nyumbani na pia wawaache polisi wafanye kazi yao ya kuwalinda wote,” Chikawe

    Kwa ufupi

    Waziri Chikawe alikiri maandamano hayo kusimamisha shughuli katika baadhi ya maeneo ikiwamo ofisi yake ambayo haikupokea wageni kwa saa kadhaa.

    Na Mbonile Burton, SAUT

    Posted Jumatano, Agosti 12, 2015

    Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe amesema wamefurahishwa na amani iliyotawala wakati wa maandamano ya kumsindikiza mgombea wa urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Edward Lowassa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua fomu juzi.

    Waziri Chikawe alisema jana kuwa alishuhudia umati mkubwa wa watu wakiimba na kucheza katika hali ya amani na hilo ni jambo zuri linalopasa kuendelea wakati wote.

    Alisema anatarajia hali hiyo itaendelea hata mikoani mgombea huyo akienda. “Tumefurahi, kulikuwa na amani ya kutosha, watu walikuwa wengi zaidi ya ilivyokuwa kwa CCM,” alisema Waziri Chikawe.

    Waziri Chikawe alikiri maandamano hayo kusimamisha shughuli katika baadhi ya maeneo ikiwamo ofisi yake ambayo haikupokea wageni kwa saa kadhaa.

    Wakati huohuo, Chikawe alionya: “Tunaomba wanasiasa na mashabiki wao wasitembee na silaha kwenye mikutano yao, waziache mahali salama nyumbani na pia wawaache polisi wafanye kazi yao ya kuwalinda wote.”

    Waziri Chikawe alisema mabomu ya machozi yanayotumika kazi yake siyo kuua au kuumiza watu bali kuzuia wasifanye vurugu.

    Hata hivyo, Waziri Chikawe alisisistiza ushiriki wa viongozi wa vyama vya siasa ni muhimu katika kufanikisha hilo.

    Alisema wanasiasa wanapaswa kujiheshimu kwa kukwepa kampeni za uchochezi na kauli zinazoweza kusababisha fujo.

    “Napenda kuchukua nafasi hii kuwaambia Watanzania kwamba tutakuwa na uchaguzi wa amani na utulivu, hiyo ndiyo dhamira yetu, lakini hilo linaweza kufanikiwa iwapo tutapata ushirikiano kutoka kwa vyama vya siasa na mashabiki (wafuasi) wao,” alisema Waziri Chikawe.

    Alisema Serikali imejipanga kuhakikishia Watanzania wanaendelea kuwa na Amani: “Tutahakikisha watu wanapiga kura kwa amani, sina wasiwasi na eneo hilo.”

    “Naomba viongozi wa siasa watusaidie, tusingependa kufikia hatua ya kupiga mabomu wakati wote…tunataka tumalize mchakato huu kwa amani,” alisema.

    Alisema dhamana ya damu ya Watanzania katika kipindi hiki iko mikononi mwake na asingependa kuona yeyote anapata maradha.

    “Viongozi wa vyama wana nafasi kubwa katika kutekeleza hilo, tunaomba wasilete vurugu, wasitishane na pia wasitumie silaha wala kufanya fujo,” alisema Waziri Chikawe.

    ReplyDelete
  13. kWANI KUNA MTU ANAESOMA GAZETI LA UHURU?

    ReplyDelete
  14. Wewe ni mwandishi wa habari gan,umaonesha hisia zako kabisa kama umeegemea upande mmoja/chama kimoja..kuwa neutral kwenye taarifa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad