Hatimaye UKAWA Wakubaliwa Kutumia Uwanja wa Jangwani Jumamosi hii Kuzindua Kampeni zao

Lowassa Akizungumza na Wahandishi wa Habari
Malalamiko ya vyama vinavyounda UKAWA ya kakatazwa kutumia uwanja wa jangwani kuzindua kampeni yameanza kufanyiwa kazi na tume ya taifa ya uchaguzi na  taarifa zilizotolewa na mkuu wa idara ya mawasiliano ya CHADEMA Bw.Tumaini Makene zimesema kuwa uzinduzi huo utafanyika kwenye uwanja huo kama ilivyokuwa imepangwa.

Bw.Makene ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano wa baraza la vijana la vyama  vinavyounda UKAWA na waandishi wa habari ambao pia viongozi hao wametumia  nafasi hiyo kuiomba tume ya uchaguzi kuwakemea viongozi na watendaji wa  serikali kufanya kazi za siasa kwa lengo la kukibeba chama tawala.

Viongozi hao wa vijana wamesema  hatua ya viongozi na watendaji wa serikali ya kujihusisha moja kwa moja na kampeni za  CCM huku wengine wakitumia rasilimali za umma  na vyombo vya dola kukandamiza vyama vya upinzani inathibitisha ukweli wa  malalamiko yao.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hawa watumishi wa serikali wanaoipendelea ccm na kukandamiza upinzani Mungu amewapiga upofu.Treni imekwisha pita haisimamishwi kwa kupunga mkono.Peopleeeesssss!

    ReplyDelete
  2. TUNAWAOMBA VIONGOZI WA UKAWA KUHUSU JANGWANI KUTAPIKA UMATI SIKIU YA JUMAMOSI TUWEKEWE CCTV SCREENS VIWANJA VYA BIAFRA KINONDONI KARUME ILALA MWEMBEYANGA TEMEKE NA ZAKHEM MBAGALA ILI MAELFU WENGINE WAWEZE KUSHUHUDIA.PIA VIPAZA SAUTI VISAMBAZWE BARABARANI TOKA FIRE HADI MAGOMENI.KAMATI YA MAANDALIZI IZINGATIE SANA USHAURI WETU.VIPAZA SAUTI VIENEZWE ANGALAU KILOMITA MOJA TOKA MAIN PODIUM NA HILI LIWE KWA ZIARA ZA MHESHIMIWA LOWASSA POPOTE TANZANIA UPENDO WALIOKUA NAO WATANZANIA KWA LOWASSA HAUNA MFANO POPOTE AFRIKA.MUNGU MBARIKI MPENDWA WETU WASAMBARATISHE WALE WOTE WENYE HUSUDA MBAYA VIROHO KISOKOROMBINGO MAPEPO WACHAFU WAKIONGOZWA NA MABWANA KIKWETE MKAPA MAGUFULI NA SAMIA.WALAANIWE WASIWEZE

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad