Hatuwezi Kuiondoa CCM Madarakani kwa wimbo wa Ufisadi, Tunahitaji watu Wenye Ushawishi

Ingekuwa ufisadi ni jambo linalowakera sana watanzania,upinzani usingekuwa na hata haja ya kufanya campaign kuiondoa CCM madarakani bali ufisadi uliofanyika katika awamu hii ya Kikwete, ulikuwa unatosha kabisa kuiondoa CCM madarakani mwaka huu.

Watanzania wangekuwa wanakerwa na ufisadi wa viongozi mithili ya wizi unaofanywa na kibaka wa kuku au simu,CCM wengeshaondoka madarakani tangu mwaka 2010.

Watanzania wako radhi waongozwe na mafisadi kuliko kuwapa nchi wapinzani kwa kwa imani potufu kuwa;

1.Upinzani hauna watu wa kutosha kuongoza hii nchi

2.Viongozi wa upinzani hawajawahi kushika dola(kuwa mawaziri n.k) hivyo hawana uzoefu wa kuongoza nchi

3.Watanzania wengi wana imani ya kijinga kuwa ni bora hawa mafisdi wa leo wakaendekea kubaki madarakani kuliko kuwapa uongozi wa nchi watu ambao wakiingia madarakani ndio kwaanza watakuwa wanaanza kujijenga hivyo wataiba zaidi kuliko hata hawa mafisadi wa CCM.

4.Bado kuna wajinga wachache wanaamini CCM ikitoka madarakani,basi amani(ukweli ni utulivu na wala si amani) itatoweka.

Hizo ndio fikra,japo ya kijinga,lakini dio zinawaongoza watanzania wengi wakiwamo wasomi wenye shahada na mashahada-kubali au ukatae huu ndio ukweli ingawa ni wa kusikitisha.

Hivyo basi,hata angesimama Dr.Slaa au Lipumba kupitia UKAWA, bado tungekuwa na wakati mgumu wa kuiondoa CCM madarakani licha ya ukweli kuwa CCM imechoka na haistahili kuendelea kuwepo madarakani.

Kwasababu hizo nne nilizotaja hapa juu, ndio maana binafsi naunga mkono ujio wa Lowassa na wana-CCM wengine ndani ya UKAWA kwani kuwepo kwao kuna punguza hofu au kwa maneno mengine kunasaidia kutoa suluhisho kwa maswala hayo manne hasa ikizingatiwa kuwa Lowassa alishawahi kuwa wazi mkuu.

Matumaini pekee ni kuwa hizo sababu nne zinaenda zikitokomea au kukosa nguvu kadri mika inavyosonga mbele ila bado tuhahitaji miaka mingine 10 kuondokana na hizi fikra potufu miongoni mwa watanzania hasa kwenye nafasi ya uraisi na kwa mawaziri wa kuongoza wizara.

Tukitaka mabadiliko ya haraka kabla ya muda huo wa hiyo miaka 10 na kuendelea kwa nafasi ya uraisi,hatuna budi kuwa-accomodate wana CCM wenye ushawishi wanaojitoa katika chama chao na zaidi tuwape nafasi katika vyama vyetu hivi vya upinzani.


Ushahidi mdogo tu kuwa kwa watanzania ufisadi kwa sio "big deal",ni kupeta katika kura za maoni za hivi karibuni kwa watuhumiwa wa Escrow na mtakuja kushangaa watu kama Chenge,Karamagi,Ngeleja wanarudi Bungeni tena kwa kura nyingi tu.

Tusijidanganye tukambeza Lowassa kuwa ni fisadi na hatoweza kutuletea ushindi kisa tu anatuhumiwa kwa ufisadi wakati watanzania ufisadi kwao sio big deal unless tunataka kuwa wapinzani wa kudumu.

Thruogh Lowassa I believe we can make those politics that seem impossible in our country to be possible at least for the first in our countrty political history.
Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe usituletee kampeni za kijinga kila mmoja ana haki ya kumpa kura amtakaye usituletee ujinga jihesabuni mko wangapi wenye akili kama zako mpeni kura zenu fisadi wenu EL Usijifanye unachambua watanzania na kutuletea sera zako zilizokosa dira ya nini kupiga kelele wakati mnasema CCM mmeisambaratisha ni mwaka wenu kuchukua Dola kipi kinakupa muhemko subirini ballot box kuamua usijipendekeza kwa watu wajifanya wayajua baina UKIWA na CCM na una haki ya kumpa kura umtakaye kama na wengine wayo haki kama yako tusiburuzane mabaliko yako CCM yanajionyesha wazi ingekuwa CCM ya zamani ya kulea mafisadi EDO angepewa kijiti bila wasiwasi hakuna ambae angepinga na hapo ndio ilikuwa mwisho wa CCM kwa bahati nzuri CCM wameotea dharuba kijiti kapewa JEMBE wenyewe mmzimia

    ReplyDelete
  2. Hoja zako hazina maana kwanza kabisa watanzania sio wajinga ila uwelewa wetu na mfumo dume tulionao ndio unatuletea shida,Watanzania wengi ukiwemo na wewe ulioandika madaa hii umuhimu wa kura yako huujui siasa kwa wabongo ni ushabiki tu kama timu za mpira, kama chama cha siasa kilikua kinapinga mafisadi walioko ccm kwa nguvu zote leo iweje Fisadi huyohuyo ahamie kwenye chama chako na unampokea kwa mbwembwe unamsafishaje ili awe mzuri kwa jamii ndio maana viongozi wenye msimamo waliliona hilo na hawakuliafiki lakini kwa vile lengo ni kuingia madarakani ndio maana mnajaribu kumtetea fisadi na kumsafisha,,,,ukweli utabaki kuwa palepale vyama vya upinzani havina msimamo na mnakatisha tamaaa,,,,,,,,hamtaingoa ccm hata siku moja hilo mkae mkijua,,,,,ni vijiji vingapi vya tanzania vinaijua chadema na cuf ushabiki uko mjini tu na baadhi ya mikoa,,,,,,,,,,mtaburuzwa sana na ccm miaka1000,,,,,

    ReplyDelete
  3. we mwandishi jidanyanye na lowasa wako, jitutumue kama mwanamke malaya anayeona umalaya kwake ni deal subilini mnyoko tu.

    ReplyDelete
  4. Nikwel kabisa ndugu mwandishi, unauna mbali mabadiliko ya kweli hayaji kwa uangalia historia ya huyu kafanya nini na nani kasababisha. cha msingi ni kuangalia utii, uadilifu na uwajibikaji katika kukuza na kuendleza nchi yetu. tukizingatia hayo tutaweza kujikwamua na umaskini.

    ReplyDelete
  5. Ndiyo mzee, we can make it.

    ReplyDelete
  6. SIYO SIRI WALA SIYO MATUSI..... WATANZANIA TUMELAANIWA KUTOKANA NA KUENDELEA KUENZI MADUDU YA ALIYETULOGA INGAWA ALISHAKUFA NA TULIMZIKA KWA MBWEMBWE NYINGI.......usibishe kishabiki, ukweli ndiyo huo

    ReplyDelete
  7. na kweli tumelaaniwa na ccm. tunalala njaa, tunalala bila umeme, tunalala bila kujua watoto wetu wataenda shule vipi, watakaa wapi LAKINI bado watu wetu wanaipenda ccm. wamelogwa na huyu mdudu ccm!

    ReplyDelete
  8. Ukweli ndio huo sio ushabiki wala nini Kama mtu alikua fisadi leo kwaje msafi urohoooo wa madaraka na walionacho wajiongezeee LOWASA alikua Fisadi ccm CHADEMA walimtukana sana leo msafiii kama sio uchu wa madaraka nini mwizi mwizi hata akiwa chadema akapata uraisi ndio atazidi kuwa fisadi.

    ReplyDelete
  9. Ebwana we itazame tazania ya ss sawa na tanzania ile tazama wasomi na angalia kila secta mm naamini km unavyosema km ni ujinga sawa tu lkn ukweli ndio huo wapizanzi inavyoonesha na waumini wao wanavyo waaminisha tanzania itakua kama pepo na hicho kitu hakiwezekani hata ashike madaraka nani hebu tukubali ukweli tu safari msafara wa mamba na kenge huwemo haiwezekani katika viongozi wa mataifa ya afrika wasikose watu km hawa hata katika familia yk ww wewe hupendi pombe lkn ndugu yako analewa na mmezaliwa tumbo moja tatizo sio ufisadi tatizo kuwapiga vita mafisadi na kuwachukulia hatua kwani fisadi hakwambii nafanya ufisadi itobidi unakiwa humju sasa nawashanga ukawa mtu washamjua ni fisadi na wamemtaja wao wenyewe baada ya kuendelea kumpiga vita ndokwanza wanampikia pilau ili aendelee kufanya ufisadi sawa na mtu muuaji hukumu yake ukampa mtu mwengine amuue jamani lazima tuwe na akili timumu hawa ukawa wanataka kuingia ikulu tu au wanataka kuleta maendeleo km wanataka kuingia ikulu tu sawa lkn km wantaka kuingia ikulu na kuleta maendeleo hilo haliwezekani kwa mtu walomchagua kwa kweli mm mpaka leo siamini kama ukawa wamefanya jambo la ajabu namna hii mm siamini sana ccm lkn ukawa wamebugi sana mtu mlompigia kelele ni fisadi hafai kuwa kiongo kwa jamii ya ya watanzania mpaka mkapika kelele awajibike leo anakua sio fisadi hii hatari inavyoonesha hata katika ukawa mna mafisadi maneno yao mdomoni yanakua mazuri lkn vitendo ni tofauti km mmekubali kuongozwa na mtu fisadi aliotoka ccm basi na nyinyi mafisadi mtu safi hakubali kuongozwa na fisadi na nawakubali sana silaa na lipumba hawa watu wameonesha kama kweli hawapendi ufisadi pamoja na mafisadi tusiwe washabiki tuangalie ukweli wa mambo ukawa hawajui nini ufisadi ndio maana wakahadaiwa na mtu fisadi kumbe lowasa hatari sana ufisadi kaufanya ndani ya ccm ss kafikia hatua mpaka wapinzani kawafanyi hivyo hivyo huyu ni mtu hatari inafikia hatua km hii watu anatuliza watu ambao hawataki kuuona ufisadi wala kuckia nadhani huyu mtu sio wa kufanyia masihara madhili kaweza kufanya hilo bc ufisadi utadumu tz mungu ibariki tz na wabariki wale wote wanaopinga ufisadi na mafisadi dah cjui ingekuwaje km lowasa angepita ccm cpati picha hali halihitaji akili nyingi ww mwenyewe muandishi jibu unalo

    ReplyDelete
  10. CHADEMA ni kampuni ya Ndesamburo ukiangaria kwa undani Mboe ni mwizi tu na tamaa ya 10 billion alizo wapa Mwizi Lwasa zitawatokea puani.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad