Jamani naombeni mnifikishie salam zangu kwa dada Doris wa Cosota
Jana usiku wa tar 6/08/2015 kwa mara ya kwanza nadhani alijikuta anasimama pembeni ya rais wa jamhuli ya muungano Mh. JK na kujibu maswali magumu kwa njia nyepesi tu.
Amepewa muda wa wiki mbili kukamilisha ripoti ya masuala yetu wasanii yakiwemo ya mirabaha na mengineyo ya wazi wa kazi na masuala ya haki.
Kwanza nimpongeze sana kwa anavyojitahidi lakini kikubwa zaidi nisisi kama wasanii tunaomba awe muwazi kabisaa katika ripoti yake kuwa
COSOTA haina ofisi ya kudumu,
COSOTA haina ghala la kuhifadhia mali zinazokamatwa baada ya misako na hii inasababisha wasifanye misako ya kukamata,
COSOTA haina sheria ya kutoza mirabaha kwa wadau bali inawaomba wachangie tu na unapomuomba mtu basi ujue ana hiari ya kutoa anacho jisikia au asitoe kabisa,
COSOTA haina ofisi mikoani
COSOTA haina wafanyakazi wa kutosha,
COSOTA ina gari moja tu je linaweza kuzunguka nchi nzima?
COSOTA inatakiwa ipate asilimia katika pesa za stika za kwenye CD ili iweze kufanya misako ya kazi feki na wizi la sivyo haina haja ya kuweka stamp za TRA na tuweke Stamp za Cosota
Pia COSOTA isimamie haki ya kazi za wanachama wake kikamilifu
Haina haja ya kumuomba mkaguzi wa hesabu wa serikali ili akaikague kosota kuwzia mwaka 1991 mpaka sasa na kujua imeingiza kiasi gani kupitia mirabaha ya sanaa ya mziki na filamu kuanzia Mabar, Mahotel, Mabasi, vituo vya Tv, vituo vya redio, kwenye mameli, ndege, libraly, cable netwok, vibanda vya video shows na sehem nyinginezo na imetoa kiasi gani kwa wahusika bali hivi sasa tunaomba tuanze mwanzo mpya kabisa
Huu ni wakati wa kusema ukweli ili nasi tule halali yetu ukificha ficha tena hali mbaya sana inakuja na mungu ndio atakae tusaidia kuyaweka bayana na yakiwa bayana itakuwa aibu kubwa sana kwa Cosota
Hizi ni salamu zangu nifikishieni jamani
Naitwa Bond
Wastara Juma on instagram