1. Meneja wa Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Estelina Sanga maarufu kwa jina la “Linah”, Doreen Noni toka Kampuni ya Panamusiq inayosimamia kazi za msanii huyo (wa kwanza kulia) akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) kuhusu udhamini wa video ya msanii wake walioupata toka Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Jebel na kufafanua zaidi juu ya uzinduzi wa video hiyo mpya itakayotambulika kwa jina la “No Stress” anayotarajia kuzindua hivi karibuni. Wa pili kulia ni msanii Linah na wa tatu ni Meneja chapa wa pombe kali SBL, Shomari Shija na kushoto ni Meneja uvumbuzi SBL , Attu Mynah. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya kampuni hiyo Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
2. Msanii maarufu wa Muziki wa kizazi kipya, Estelina Sanga maarufu kama “Linah” (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hawapo pichani juu ya Video yake mpya ijulikanayo kama” No Stress” inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni chini ya udhamini wa Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Jebel Coconut, katikati ni Meneja chapa pombe kali toka SBL, Shomari Shija na Meneja uvumbuzi SBL, Attu Mynah. Tukio hilo limefanyika makao makuu ya kampuni hiyo Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
3. Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Estelina Sanga maarufu kama “Linah” (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hawapo pichani juu ya ujio wa video yake mpya itakayokwenda kwa jina la “No Strees” ambayo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni kwa udhamini wa Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Jebel Coconut ambapo yeye ni balozi wa Kinywaji hicho. (Wa pili) ni Meneja chapa wa pombe kali SBL, Shomari Shija, Mkutano huo ulifanyika makao makuu ya Kampuni hiyo, Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
4. Meneja chapa wa pombe kali SBL, Shomari Shija (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya udhamini wa uzinduzi wa video mpya ya msanii Estelina Sanga “Linah” itakayokwenda kwa jina la “No Stress” kupitia kinywaji chake cha Jebel Coconut. Kushoto ni Meneja uvumbuzi SBL, Attu Mynah, na kulia ni msanii Linah. Tukio hilo lilifanyika makao makuu ya SBL Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
5. Meneja chapa pombe kali toka SBL, Shomari Shija (kushoto) akiongea na waandishi wa habari hawapo Pichani juu ya udhamini wa uzinduzi wa video mpya ya msanii maarufu Estelina Sanga a.k.a” Linah”(katikati) wimbo ukijulikana kama “No Stress”. Wimbo huo umedhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Jebel Coconut ambapo msanii huyo ni balozi. (wa kwanza kulia) ni Doreen Noni Meneja wa msanii huyo toka Kampuni ya Panamusiq inayosimamia kazi za Linah. Tukio hilo lilifanyika makao makuu ya SBL Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
6. Meneja uvumbuzi SBL, Attu Mynah, (kushoto) akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu udhamini wa video mpya ya msanii “Linah” kupitia chapa ya Jebel coconut toka SBL chapa ambayo msanii huyo ni balozi. Video hiyo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni na itakwenda kwa jina la “No Stress” (Wa pili) ni msanii Linah na wa kwanza kulia ni Meneja wa msanii huyo Doreen Noni toka kampuni ya Panamusiq inayosimamia kazi za msanii huyo. (Wa pili) kushoto ni Meneja chapa pombe kali toka SBL, Shomari Shija.
7. Meneja chapa pombe kali toka SBL, Shomari Shija (kushoto) akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya udhamini wa uzinduzi wa video mpya ya msanii maarufu Estelina Sanga a.k.a Linah” (katikati) itakayojulikana kwa jina la “No Stress”. Udhamnini wa msanii huyo unafuatia ahadi ya Kampuni ya bia ya Serengeti kusapoti kazi zake baada ya msanii huyo kupata mkataba wa ubalozi wa kinywaji cha Jebel Coconut toka SBL. (Kushoto) ni Meneja wa msanii huyo Doreen Noni toka Kampuni ya Panamusiq inayosimamia kazi za msanii huyo. Tukio hilo lilifanyika makao makuu ya SBL Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Jebel Coconut imetangaza rasmi siku ya leo dhamira yake ya kudhamini uzinduzi wa video mpya ya msanii Estelinah Sanga maarufu kwa jina la kisanii “Linah” itakayo kwenda kwa jina la “No Stress”.
Video ya wimbo huo imefanyika nchini Kenya na Afrika ya kusini ambapo kwa kushirikiana na menejimenti ya msanii huyo, SBL imeweza kudhamini utengenezaji wa video hiyo ambayo hadi sasa imeshakamilika huku Kampuni hiyo ikisubiria kuizindua rasmi kwa wananchi.
Hatua ya SBL kudhamini video ya wimbo huo ni njia mojawapo ya Kampuni hiyo kutambua sanaa ya muziki hapa nchini ambapo pia hapo awali Kampuni hiyo iliahidi kumsapoti msanii huyo mara baada ya kupata mkataba wa mwaka mmoja wa kuwa balozi wa kinywaji cha Kampuni hiyo cha Jebel coconut.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utoaji wa taarifa hiyo kwa umma, Meneja Uvumbuzi wa kampuni hiyo Attu Mynah alisema “Kampuni ya bia ya Serengeti inatambua umuhimu wa Sanaa ya muziki hapa nchini na siku zote inalenga kumuwezesha msanii aweze kufikia malengo ya ndoto zake. Tumeamua kudhamini utengenezaji na uzinduzi wa video ya wimbo wa msanii Linah kwa kuwa tunatambua uwezo wake na tungependa afike mbali zaidi kimuziki”.
, alisema “Tunafuraha kwa kuwa Kinywaji chetu cha Jebel coconut kinaendelea kujizolea mashabiki wengi kupitia ubalozi wake ambapo ameendelea kuitangaza chapa hii sehemu mbalimbali za Tanzania. Kama SBL tunajivunia kudhamini baadhi ya kazi zake na ni matumaini yetu kuwa kupitia udhamini huu ataendelea kufanya vizuri zaidi katika ngazi za kimataifa”.
Jebel coconut ni aina ya pombe kali yenye ujazo wa 250ml inayotengenezwa nchini Tanzania na Kampuni ya bia ya Serengeti ambayo imebuniwa na kutengenezwa kwa ladha ya nazi ambazo zinapatikana kwa wingi hapa nchini. Jebel pia ni kati ya pombe kali zaidi ya 10 za kimataifa zinazosambazwa na kampuni ya bia ya Serengeti huku walengwa wa kinywaji hiki wakiwa ni watu wazima na wenye umri wa kati.
**MWISHO**
Kampuni ya Bia ya Serengeti Kudhamini Uzinduzi wa Video Mpya ya Msanii Linah Sanga
0
August 03, 2015
Tags