Kanisa Lagoma Kumbatiza Mtoto wa Aunt Ezekiel

Kanisa Katoliki limemzuia staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel kumbatiza mwanaye kutokana na kutokidhi matakwa ya kanisa.

Tukio hilo limetokea hivi karibuni mara baada ya mwigizaji huyo ambaye imani yake ni ya Kiislamu, kutaka kumbatiza mwanaye huyo ambaye baba yake ( Moze Iyobo) ni Mkatoliki.

“Alikuwa amejipanga kumbatiza Kikristo kutokana na imani ya baba mtoto wake lakini alipokutana na padri Paul Ruwaaich wa Parokia ya Uparo Moshi aliyekuwa Dar kikazi akamtaka akaanzie kusali kwenye Jumuiya Ndogondogo (mtaani kwake), abadilishe dini ndipo mtoto huyo abatizwe kwani ndizo taratibu za Kanisa Katoliki.

“Alipopewa sharti hilo, lilikuwa gumu kwa Aunt, ikabisi ageuze zake,” kilisema chanzo chetu.

Mwanahabari wetu alipomuuliza Aunt kuhusu suala hilo, alisema amebaki njia panda na anatafakari cha kufanya.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyo si mme wako, mtoto mpeleke madrasa

    ReplyDelete
  2. Kanisa Katoliki linatoa mamlaka kamili kwa Kanisa Mahalia. Kanisa Mahalia kwa ishu hii ni Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Jimbo Kuu la Dar es Salaam lina taratibu zake kuhusu ubatizo wa watoto wachanga. Taratibu zinaanzia kwenye Jumuiya ambayo wazazi wa huyo mtoto wanajumuika. HAKUNA NJIA MKATO.

    ReplyDelete
  3. kwa mila zetu hata kama huyo si mumeo lakini ni mtoto wake.anachukua ubini wa baba,kabila la baba na dini ya baba.kuwa makini katika kumlea mtoto kiimani..msimyumbishe.wapo wamama wengi wamekutana na changamoto kama yako..tunashiriki nao kwenye jumuiya kwa ajili tu ya makuzi mema ya mtoto kiimani.weka interest zako pembeni na hakikisha mtoto anakua akiwa na hofu ya Mungu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad