MUUNGANO wa wapiga kura Tanzania (TANVU), umeiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumchukulia hatua, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, kwa kitendo alichokifanya kuvitukana vyama vya upinzani kwa kuwaita viongozi na wanachama wake malofa, vibaka na wapumbavu.
Kauli ya TANVU inakuja ikiwa ni siku chache baada ya Mkapa kutoa maneno ya kuvihadaa vyama vya upinzani wakati Chama cha Mapinduzi (CCM) kilipokuwa kinazindua kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika kwenye viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam.
Pia muungano huo umekipatia CCM muda wa siku saba kuanzia leo kuwaomba radhi watanzania kwa kutumia Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu nchini (SHIVYAWATA) kwenye uzinduzi wa kampeni hizo huku kikitambua ni makosa kisheria kwa vyama vya siasa kutumia Taasisi zisizokuwa za serikali kwenye kampeni za uchaguzi.
Kauli hiyo ya TANVU imetolewa leo jijini Mwanza na Rais wake, Militon Lutabanana wakati akizungumza na wandishi juu ya hali ya kisiasa nchini, demokrasia na kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Amesema hatua ya SHIVYAWATA kushiriki kwenye uzinduzi wa kampeni za kisiasa za CCM ni makosa kwa kuwa kwa mujibu wa sheria za nchi taasisi yoyote isiyo ya serikali hairuhusiwi kujiingiza kwenye shughuli za kisiasa.
“Kwa kitendo hicho wote wanamakosa CCM na SHIVYAWATA lakini kama CCM haitaomba radhi tutatoa tamko lingine ambalo sisi kama muungano wa wapiga kura nchini hatupendi tufike huko,” amesema na kuongeza.
“Tunaiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi itende haki kwa kumchukulia hatua stahiki Rais Mkapa kama ambavyo jana tumeshuhudia aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Laurence Masha alivyoshughulikiwa,” amesema.
Amesema wapiga kura hawahitaji kusikia matusi wala vijembe kutoka kwa wagombea, viongozi au wanachama wa vyama vya siasa wanachotaka kusikia ni sera za vyama hivyo vya siasa na sio vinginevyo.
“Tunawaomba makada wa CCM waache kuendesha kampeni kwa mabavu, Magufuli (John) hatuna tatizo naye tunamshauri asikubali kuombewa kura na watu wanaotumia matusi,” amesema.
Aliongeza kuwa kitendo cha Rais Mkapa kutoa lugha za matusi kitamharibia mgombea wa CCM na kumpunguzia idadi ya kura kwa kuwa yeye alikuwa kama mdhamini wake kwa wapiga kura.
KIMENUKA! Wananchi Ambao Ndio Wapiga Kura Wamtaka Rais Mstaafu Benjamin Mkapa Aombe Msamaha
6
August 26, 2015
Tags
msi zingue watu hata akiomba msamaha is to late kila mtu atachagua mgombe amtakae hao UKAWA ndio wanataka na wewe muandishi mbona mi na piga kura na sijasema aombe msamaha najua kura yangu Nampa nani hatuhitaji msamaha wake. si waache kupiga kura kwani lazima.
ReplyDeleteAombe radhi haraka maana baada ya ufisadi wote waliotufanyia wameona waongeze na matusi kama kiongozi unafundisha nini wananchi na watoto wadogo
ReplyDeleteacha ujinga na wewe tena wewe ni mburura namba moja, hivi ni nani mtumwa katika nchi hii? kama ni mtumwa labda wewe na familia yako, huyo sumaye atukomboe katika lipi wakati nchi haina utumwa? acheni ushabiki wa kipumbavu shenzi zako kabisa
Deletekasema kweli tucjifanye hatufahamu au kupindisha maneno huwezi kuwatukana watanzania kuwa hawapo huru yaani ni watumwa sasa mtu anaitwa mtumwa anaona kawaida tu mm hapa ndo nashangaa kweli hawa watu wanata kutugomboa na nn ? watake wctake tanzania ipo huru hawa watu wanataka madaraka tu ndo hawaangalii juhudi yyte ya serikali
ReplyDeleteSISI TUNASIKITIKA MATUSI ALIYOTOA MKAPA HAYO HAYO HUYAZUNGUMZI IILA UNASEMA KASEMA KWELIKWA KUA HUYAJUI MATUSI POKEA HILO KUMAMAYO.LIHIFADHI AU MPELEKEE MKAPA
Deleteumenena
Delete