Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amesema kwamba chama Chama Mapinduzi kinatarajia kupata ushindi mnono katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwezi oktoba mwaka 2015.
Akizungumza na Wanachama wa CCM leo katika ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijini Dar es salaam mara baada ya mgombea wake wa Urais Dk.John Pombe Magufuli kuchukua fomu ya kugombea urais tume ya Taifa ya Uchaguzi amesema kwamba chama hicho kwa bahati nzuri mwaka huu kinashindana na makapi yake ambayo kamwe hayawezi kuishinda CCM.
“Nchi yetu inakwenda kwenye uchaguzi ikiwa na wagombea na makapi, sasa kati ya mgombea na makapi nani mshindi?” Amehoji Kinana
Ameongeza kuwa kila mwanachama akitengwa na CCM mahala pake ni wapi? Huku mamia ya wananchi wakijibu ‘Chadema’ kwa sauti ya juu.
Naye Mwenyekiti wa CCM Dk. Jakaya Kikwete amesema kwamba serikali ya CCM imefanya mambo mengi ya Maendeleo na mwaka huu wana waahidi watanzania ushindi wa kishindo.
Kwa upande wa Mgombea Urais wa CCM Dk. John Magufuli amesema kwamba ikiwa atachaguliwa kuwa rais anakwenda kufanya wananchi walicho mtuma kwa kuwa shida za watanzania anazifahamu huku akirejea kauli yake Maendeleo hayana chama.
Hivi karibuni chama cha Mapinduzi kimepata mtikisiko mkubwa kufuatia wanachama wake kuhama chama hicho na kutimkia Upinzani hususani Chama cha Chadema akiwemo Waziri mkuu wa Zamani Edward Lowassa, Makongoro Mahanga, James Lembeli pamoja na Ester Bulaya
Ccm in ugonjwa kama ukoma
ReplyDeleteHuyo Lowasa ni CCM damu, hawezi kubadilika ghafla kiasi hicho, na hata akishinda bado ni KAPI LA CCM.....upo hapo?
Deletesi mpaka muibe kura nyie oteni ndoto,mtashangazwa safari hii , nchi siyo yenu lazima mkae tumechoka,miaka 50 dawa hakuna maospitalini,wakina mama wajawazito wana lala chini maospitali na hayo ni machache tu.
ReplyDeleteNchi sio yao wapeleke kwao Kongo kabla ya uchaguzi October 25 halafu mtabakia wenyewe mtachukua nchi yenu kiulaini miaka 50 mlikuwa wapi kuwahamisha
DeleteDemokrasi sio kutoleana maneno ya kifedhuli na dharau nyie subirini October 25 mtanyooka tuu kura mmeisha jiibia wenyewe kwa kumsaliti Dr. Slaa
ReplyDeletemtajuta ccm mbele kwa mbele
ReplyDeleteWananchi mnataka changes but hamjui nani anafaa ebu angalia ata katiba ya jamuhuri hamuijui then mnapiga kelele tatizo mnafuata mkumbo,
ReplyDeleteWatanzania ni nani aliwaroga mpaka mkawa kila siku ccm .MABADILIKO NI LAZIMA KWA BINADAMU PIGA TEKE CCM WEKA UKAWA
ReplyDelete