Kutoka Diamond: Mapokezi ya Magufuli baada ya kurejesha fomu NEC

Kikwete: CCM haibahatishi, ni chama kikubwa kinawajua watu wake vizuri, sasa nataka nimlete ndugu Magufuli. Anaimbisha wimbo wa kumkaribisha Magufuli. Watu wajue leo CCM ndio imeanza, kama walikuwa wanchukua picha na kuunganisha kwenye computer, sasa zinakuja picha za kweli. John Magufuli ndio Rais na Samia ndio makamu


Magufuli: CCM oyeee, Ali nselema...

Sikutegemea kama patakua na wananchi wakereketwa ndani ya mioyo yao na wenye nyuso za furaha na wamependeza kweli kuhudhuria muda huu. Nimeomba kukutana na wazee wa Dar es Salaam kwa niaba ya wazee wa Tanzania, nafahamu ukitaka kupata busara, utapata kwa wazee. Uzuri leo wazee wamesindikizwa na vijana, ninawashukuru sana. Kabla sijaendelea niwashukuru wazee na wananchi wa Dar kwa kunikaribisha, niliingia mara ya kwanza 1978 wakati naenda kujiunga kidato cha tano, nilikaa siku mbili kisha nikaelekea Iringa. Nilipokuja tena kwa masomo ya chuo kikuu sijawahi kuulizwa dini wala kabila langu. Ninawashukuru sana wana-Dar es Salaam na watanzania.

Ninyi wazee wa Dar mna historia kubwa katika taifa hili, baba wa taifa wakati akiwa kwenye harakati za kudai uhuru alifika Dar es Salaam na akakutaa na wazee, mkamuombea dua na kumbariki na hatimae tukapata uhuru bila kumwaga damu, wakati wa Idd Amin, Nyerere alikutana tena na wazee wa Dar es Salaam, akazungumza nao na mkampa uwezo wa kwenda kushina na yeye akatamka nia tunayo, uwezo tunao. Idd Amin akakimbilia huko alipokimbilia.

Leo wazee wangu nami nimewaita ili nije nipate busara zenu na dua zenu kwa sababu natambua nikizungumza na wazee wa Dar es Salaam mambo yangu yatakua safi kabisa. Mara baada ya kuteuliwa na kupata kura nyingi kabisa na baada ya kumpata Mh Samia kuteuliwa nafasi ya makamu urais kwa mara ya kwanza. Ninachowaomba watanzania na Dar kwa ujumla tuwe wamoja, kura zimeshamalizika, sasa jukumu letu kubwa tulilonalo ni kuhahakikisha tunafanya kampeni nyumba kwa nyuma, kutanda kwa kitanda, uvungu kwa uvungu mpaka tunashinda. Ndugu zangu wa Dar leo haya nilikuwa nachomekea tu, kwa sababu nafahamu tar 23 pale Jagwani itakuwa ndio siku yenyewe ya kuzungumza lakini niwaambie, mimi ninatosha kila mahali. Mbele natosha, nyuma natosha, ubavuni natosha na kila mahali natosha. Shida za wana-Dar es Salaam nazifahamu na kwa bahati nzuri katika uzoefu wa miaka 20 niliokaa serikali, sijawahi kushindwa mahali, mtuamini na hatutawaangusha. Mungu awabariki sana, yatakayokuja kwetu kama changamoto tutayakamilisha kwa nguvu ya hali ya juu. Na vyama vishindwe na vilegee.

Ali nselema, CCM nselema........

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MHESHIMIWA ULIPOIMBA ALINSELEMA ULISAHAU AU ULIFANYA MAKUSUDI KULIACHA NENO MOJA NALO NI MCHAKA MCHAKA.NI NENO MUHIMU SANA TENA LA USHINDI.PIA KILE KIBWAGIZO ULICHOKIPIGIA MAKOFI SANA PALE DODOMA;TUNA IMANI NA LOWASSA,OYA OYA OYAAA.KWA KUSAHAU HIVYO INAKUBIDI UITISHE KIKAO KINGINE TENA DIAMOND.HAPO TUTAKUELEWA.

    ReplyDelete
  2. Magufuli oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Haya kazi kwako magufuli angalia wasije wakiyafungua yote mana funguo hata za kuchonga zipo

    ReplyDelete
  4. Naanza kukuonea huruma Ndugu POMBE.Kwani hivi mbona simsikii MKAPA aliyekuja na jina lako toka MFUKONI KWAKE?Hauna ujanja Huna pa KUTOKEA.TUNA IMANI NA LOWASSA OYA OYA OYAAAAA.Kama CHATO Mabali basi jibanze kwako ADA ESTATE.

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe sema unaimani na lowasa so ntuna unamchanganya na nani wakati unaenda kupiga kura peke yako

      Delete
  5. mwenye akili timamu na mzalendo wa nchi hii awezi kumshabikia Lowasa. bali lazima atafakali. nanukuu, tunaweka vyama vingi ili CCM isilale, ila si ngazi ya RAIS. Kwa wabunge sawa, RAIS lazima atoke chama tawala. Mi sio shabiki wa chama chochote, ila busara itawale, wala mhe. Magufuri anifahamu! MAGUFURI ANAFAA KWA KILA MTU. WAZEMBE, WAPENDA VYA KUPEWA, NDIYO WANASEMA WANAMPENDA ROWASA ETI ANAOGOPA UMASKINI. ALIPOKUWA WAZIRI MKUU, UTAJIRI MLIPATA?

    ReplyDelete
  6. ccm iko mahututi; ccm ina ukoma; ccm ina ugonjwa wa ukimwi wa kula rusha! Na hii haizuiliki tena ndani ya ccm! ccm kwa heri ya kuonana kama tulivyomuaga KANU na UNIP! Kwa heri ccm; kwa heri nape; kwa heri kinana kwa heri mangula! Kwa heri ya kuonana!

    ReplyDelete
  7. Mwehu karopoka chini ya Kikwete ulitegemea nini,wee makonda shika adabu

    ReplyDelete
  8. Kiila Mzee nkiwepo mimi tulipewa posho ya shilingi 20,000 lakini niliona mwenzetu mmoja kalipwa 100,0000,eti ni muhamasishaji posho nje nje Diamond jirani kabisa na Makao makuu ya Takukuru na wengine tulikua nao akiwemo mkubwa Wao.Mwaka huu kazi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad