Kwa Hili Alilolifanya Diamond, Litamgharimu Sana Katika Safari Yake ya Kimuziki

Diamond Platnumz
Diamond platnumz kaonesha wazi msimamo wake katika mgonbea anayemtaka yeye. Sipingani na maamuzi yake, ila naona kama alikurupuka kufanya maamuzi hayo. Diamond angetambua kuwa washabiki wake wengi wanaompa support hawapo katika mrengo anaoushabikia yeye. 

Nimepitia baadhi ya comments za followers wake na kugundua kuwa 90% wamekuwa disappointed sana na alichokionesha.

Halafu ukiangalia ni kama wametumwa hivi baada ya ile hafla yao na mheshimiwa. Maana baada ya pale wasanii kibao wamekurupuka kuonesha support kwa Magufuli.

Kinachoendelea saiv ni kwamba washabiki wameanzisha kampeni ya kutomsapport tena Diamond kwa kuacha kumpigia kura katika tunzo anazoshindania.

Namuonea huruma sana..

Top Post Ad

Below Post Ad