LOWASSA Alitofautiana na Misimamo ya CCM Hata Kabla Hajaenguliwa Kugombea Uraisi Kwanini?

Mgogoro au tofauti kati ya Lowassa na chama cha awali ulionekana mapema hata kabla ya kufanyiwa mizengwe katika uchaguzi wa mgombea uraisi wa chama hicho kutokana na misimamo yake.

1. Alikubali kuwajibika kisiasa jambo ambalo ni nadra kwa kiongonzi wa CCM

2. Alitamka hadharani kutofautiana na kipaumbele cha "kilimo kwanza" yeye alitaka "elimu kwanza" .

3. Alidai ajira ya vijana ni "bomu linalosubiri kulipuka" muda wowote, wakubwa wake wakamnunia wakidai mambo yako shwari.

 4. Anachukizwa na umasikini watanzania wenzake walidai hali ya uchumi ni nzuri labda kwa wenye kuvaa miwani ya mbao.

5. Anaamini katika mabadiliko sasa (Time 4 Change now) wenziwe BRN . Toa maoni yako na kama yapo niliyoyasahau ongeza tafadhali.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. We HR acha uzembe na uvivu wa kufikiri sasa ulitaka ashabikie hayo madudu na kuyaunga mkono yani naona na wewe ndo walewale waliokunywa uji wa mgongwa matokeo yake unajua kifuatacho ni nini. Sijui ni nini tatizo yani kuna watu wao nadhani washarogwa na ccm utafikiri mnaboa kiukweli inafikia mahala ccm mnaitukuza utafikiri ndo Mungu wenu watanzania wanachokitaka kwa hivi sasa ni kuondokana na madudu haya ya ki ccm. Tatizo kuna baadhi ya watumishi walishazoea kutumika vibaya ndo maana hata kama mwajiri akimwagiza kwa mambo ya kipumbavu kinyume na utaratibu lazima watatekeleza sababu kwao kutekeleza makosa ishakuwa tabia na sehemu ya maisha yao. Badilika jamaa soma alama za nyakati hata picha inayoendelea nayo inakuwa ngumu kuona na kuielewa? Amka toka usingizini....Jamii isiyokubali mabadiliko kamwe haiwezi pata maendeleo ya kweli yanayooneka si yale ya kwenye hotuba za kila mwisho wa mwezi.

    ReplyDelete
  2. Mnafiki mkubwa huyo, eti anachukizwa na umasikini......!! ndio sababu ilomfanya ajilimbikizie mali yeye tu??? Alifanya nini kusaidia hao masikini?? Maneno ya kuchukizwa na umasikini ayaseme Paul Makonda angalau kaonesha kweli anakerwa na umasikini, au Reginald Mengi ndio anakerwa na umasikini akaanzisha mashindano ya kutweet wazo la biashara, sio yeye 'mroho'......ikulu ataiota usingizini

    ReplyDelete
  3. Acha kutuzingua Mabanga... Utawala gani wa sheria- wa kuogopa kusimamia kile unachokiami? Acha kukariiii/ sidhani kama unahitaji kwenda dara la 3 ndiyo ujue kipi kinatangulia kati ya kilimo kwanza na Elimu kwanza....Lowasa anachukia umasikini ndiyo maana alianzisha hizi shule za kata ili vijana wa familia za walala hoi wapate mwanga wa kutatuta changamoto zinazowakabili kwenye maisha yao ya kila siku..na hao vijana ulio waona kwa Makonda ni matunda ya hizo shule za kata...au ulitaka awapatie pesa ndiyo ujue anauchukia umasikini?
    Tatizo siyo Lowasa......tazizo Nyota....mtaisoma #

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad