Akizungumza na wafuasi wa Chadema pia UKAWA katika ofisi za Chadema mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania urais kupitia chama hicho jana mchana, Lowassa alisema;
“Rafiki yangu Jakaya Kikwete ameuharibu uchumi wa nchi yetu,”
“Wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani kilo ya sukari ilikuwa Sh. 600 leo ni Sh. 2,300. Mchele ulikuwa Sh. 550 leo ni Sh. 2,300. Sembe ilikuwa Sh. 250 leo ni Sh. 1,200.”
Aidha Lowassa alisema, katika kipindi cha utawala wa Rais Kikwete ndipo Tembo na kila aina ya wanyama wameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia ya Tanzania.
“Katika utawala wa Rais Kikwete, Tembo wameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia duniani kote.
“Kila aina ya mnyama ameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi yetu. Nitaijenga serikali yenye uchumi kwa speed (kasi), ambaye hawezi akae pembeni,” alisema Lowassa.
Angalia video hii hapo chini umsikie Lowassa akitoa tuhuma hizi.:-
Mheshimiwa, hayo ni maneno tu. Hata kwenye kanga yapo. Si tunachotaka amani yetu iendelee kudumu. Hatutaki purukushani.
ReplyDeleteWakati JK anaharibu uchumi yeye Edo alikuwa wapi?
ReplyDeleteHuyo Lowasa mwenyewe ndio alochangia yote hayo, tunamshangaa anavyoutia ulimi wake puani, anatafuta pakutokea..... atasubiri sana, ikulu ataiona akiende sokoni ferry kununua samaki.........Mr. Alcohol inamhusu
ReplyDeleteWakat anauharibu yeye alikua wapo?
ReplyDeleteYeye akijalikua wap?
ReplyDeleteWakati anauharibu yeye alikua wapi?
ReplyDeleteDah kasahau shoti alizoitia serikali
ReplyDeleteMzee kachoka hajui alikuwa mojawapo Katika kuharibu uchumi
ReplyDeleteKama ulikuwa na mapenzi na watanzania wenzako kwnn usilikemee hilo kipindi cha uwaziri wako!wacha kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa! Cc c wanafki kama hao walio kuita fisadi kipindi upo ccm Leo wanakuita msafi.
ReplyDeletehamujui chochote nyiee, ebu fungeni midomo yenu hiyo
ReplyDeleteLowasa alikuwa sehemu ya serikali kwa kipindi chote cha utawala wa kikwete. Kitu cha kushangaza Lowasa hazungumzii ufisadi ambao Ni chanzo kiubwa cha umasikini. Kwake ndio source ya kipato hence Hana moral authority kukemea wezi.
ReplyDeleteLowasa hajakua waziri kwa kipindi chote cha jk bali ni kwa miaka miwili tu (2) na baada ya tuhuma ya richmond alipotaka kuuvunja mkataba mh. jk akakataa! akajiengua kwa kukilinda chama na serikali. Lakini baada ya hapo tumeshuhudia ufisadi wa hali ya juu sana ndani ya ccm na serikali yake kama epa, escrow, wanyama kuuwawa na mambo mengine mengi. SO MUACHENI EDO ALONE OK!
ReplyDelete