Lowassa Apewa Onyo na Kamanda Kova...Staili yake ya Kampeni ya Kuwatembelea Wananchi Kwa Kushtukiza yaweza Kutumiwa na Maadui Kumdhuru

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemtahadharisha mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema Edward Lowassa kuwa kampeni alizoanza kwa kuyatembelea makundi kadhaa zinaweza kutumiwa na maadui wa kisiasa kumdhuru.

Hata hivyo, wanasiasa wametakiwa kufuata ratiba ya kampeni kwa kuzingatia mwongozo wa Tume ya Uchaguzi (NEC) ili kulisaidia jeshi hilo kukabiliana na vitendo viovu.

Onyo hilo limetolewa ikiwa ni siku ya pili tangu Lowassa na mgombea mwenza Juma Duni Haji walipoanza kuwatembelea wananchi huku wakitumia usafiri wa umma.

Kwa kutumia staili hiyo, leo Lowassa akiwa na Duni Haji wametembelea maeneo ya Tandika, Tandale na Kariakoo jijini Dar.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema ziara iliyofanywa leo maeneo ya Swahili, Kariakoo zimesababisha mikusanyiko isiyo ya lazima na kusimamisha shughuli za maendeleo.

Baada ya CCM kuzindua kampeni zake mwishoni mwa juma lililopita viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam, Chadema nacho kinajiandaa kufanya hivyo Agosti 29 maeneo hayohayo.

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kova km ni kiziw kipofu bubu mleavu wa miguu mikono na pia uwe ndondocha pamoja na yote hayo km unayo basi unajua fika km kule Amerika wenzetu wameeendele na wanazo shughuli za maendeleo kuliko sisi na pia wakat wa kampeni candidaat wanatembea mitaani kutafuta wapiga kura. mbali na yote hayo Obama mwenyewe pia huwa anatembea mitaani hata hivyo pa oja na mikusanyiko yote hiyo na shughul za maendeleo kusimama kwa muda basi hakuna taasisi yoyote iliyo lalamika,

    ReplyDelete
  2. BWANA KOVA NA WEWE PIA MPE ONYO MKAPA ALIYEWATUKANA WATANZANIA; AU UMPE ONYO MAGUFULI ALIYEZIDISHA DAKIKA 45 ZA MKUTANO WA KAMPENI! FAIR ENOUGH, RIGHT!?

    ReplyDelete
  3. HUNA LOLOTE VIVU WENU NA MACCM YAKO,TUTAMLINDA SISI MWENYEWE, HATA MSIPOKUJA KWANZA HATUWAHITA KALINDENI CCM

    ReplyDelete
  4. Mmeanza hampigiwi ccm mnacheza ngoma siyo yenu kweli nyie fystu we cova subiri

    ReplyDelete
  5. Lowassa.kama raia mwingine yeyote anavunja sheria gani kutembelea wananchi.Policcm acheni unazi wenu,ICC inawafuatilia kwa karibu sana

    ReplyDelete
  6. Hii ndio inavyotakiwa staili za kutegana zipigwe marufuku UKAWA wameishiwa kwani kina Mbowe wanataka wamtoe kafara huyu mzee huwezi kumuexpose mgombea urasi kirahisi eti anataka kujua shida za wananchi na kuhatarisha maisha yake kama hakuna njama zimepangwa ni nini ili adhurike wasingizie CCM waje waanze kutuletea balaa na kudai ushindi ulikuwa wao hawa watu wakuogopwa kuliko ukimwi

    ReplyDelete
  7. Lowasaa amevunja SHERIA ipi? Katiba iliyopo na ile RASIMU ya WARIOBA zote zinasema KILA MTANZANIA ANA HAKI NA UHURU WA KUJUMUIKA na wenzake! Ebo!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad