Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa taarifa kuhusu utaratibu wa Mgombea wa UKAWA, Edward Lowassa kuchukua Fomu za Urais katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Akitoa taarifa hizo mbele ya waandishi wa habari leo mchana, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, ndg Salum Mwalimu ambaye kwa sasa anakaimu nafasi ya Katibu Mkuu wa Chadema amesema Mh. Lowassa atachukua fomu hizo Jumatatu ya tarehe 10, Agosti 2015, saa tatu kamili asubuhi.
Mwalimu amesema msafara wa Lowassa utaanzia katika ofisi za CUF zilizopo Buguruni ambapo utaelekea ofisi za Tume ya Uchaguzi kwa ajili ya Kuchukua fomu.
Baada ya zoezi la kuchukua fomu, msafara huo utaelekea makao makuu ya CHADEMA Yaliyoko Kinondoni ambapo kutakuwa na shamrashamra kidogo.
Hapa kuna sentensi 14 ambazo mwalimu amezitamka wakati akiongea na waandishi wa habari.
1.Tupo ktk Kipindi cha Uchaguzi na Wagombea Urais wa Z'bar na TZ Bara tayari tumewatangaza'-
2.Tarehe 10 Mgombea Urais wa TZ ataongozana na Mgombea mwenza wake kwenda kuchukua Fomu NEC.
3.Mh. LOWASSA atasindikizwa na Viongozi Mbalimbali wakubwa wa Vyama vinavyounda Umoja wa UKAWA.
4.Zoezi la Uchukuaji wa Fomu msafara utaanzia Ofisi za CUF Buguruni kuelekea Tume ya Uchaguzi.
5.Msafara utaishia Ofisi za CHADEMA K'ndoni ambapo kutakuwa na shamrashamra kidogo.
6.Mh. LOWASSA atazunguka Mikoani kutafuta wadhamini, Watz wana hamu kumuona LOWASSA akiwa na combat ya CDM.
7.Mtaniwia radhi kwamba hatoweza kuzunguka nchi nzima, tutatangaza maeneo ambayo atapita.
8.Baada ya Uzinduzi wa Kampeni Dar, LOWASSA atapita Majimbo yote kama alivyoahidi.
9.LOWASSA Tarehe 13 atashiriki na Viongozi wengine kwenye Mazishi ya Mzee KISUMO Mkoa wa K'njaro.
10.Hatuwezi kuwazuia watu wanaotaka kumsindikiza LOWASSA kuchukua Fomu Ofisi za NEC.
11.Kazi ya kugawanya Majimbo ya Ubunge imekamilika, kazi imekamilika salama na kwa amani.
12.Kuna jambo linaendelea watu wanaambiwa wakusanye Kadi zao za Kupigia Kura.
13.Yoyote anayeambiwa atoe kadi au atoe namba ya Kadi yake ya Kupigia Kura akatae.
14.UKAWA haijayumba kwa namna yoyote kwa kuondoka kwa Prof. LIPUMBA, tunasonga mbele.
Lowassa Kuchukua Fomu za Urais Katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jumatatu Saa tatu Kamili Asubuhi.
12
August 08, 2015
Tags
Kwani lowasa ndio nani..!?
ReplyDeletePresident
DeleteWewe mtoa maoni? Uko duniani hapa? Uko Tanzania hii ya leo kweli? Hujui Lowassa ni na Nani? Ngoja nikujibu hapa chini:
ReplyDelete(a) Lowassa ni Raisi wa awamu ya nne na Raisi wa amamu ya tano kwa kipindi cha miaka mingine KUMI tu. Kwa nini nasema hivi? Hapa chini ni 10 tu kati ya sababu 300!
(a.1) kwanza tanzania ilikuwa na Raisi wa awamu ya nne?
(a-2) tanzania ilikuwa na mtu wa kutembea au kutalii dunia ni nzima - mtalii
(a-3) tanzania ilikuwa na mtu asiyekuwa na maamuzi magumu
(a-4) tanzania ilikuwa na mtu ambaye ameona mauaji ya kinyama yanfanywa na kakaa kimya: akina Mvungi? Maelezo yalikuwepo? Waadnishi wa habari- k.m Mwangosi - kulikuwa na maelezo?
(a_5) tanzania imeona hata madereva waliamu kugoma - ulishawahi kuona serikali imedharau wati wake kama hivyo?
(a- 6) tanzania ilikuwa na mtu aliyekuwa mswahili sana ikulu!
(a-7) tanzania iliuwa rasilimali zake zote kwa wageni - wakifikiri watanzania wenyewe hawataweza kuzisimamia
(a-8) tanzania ilikuwa na mtu ikulu aliyehakikisha kwamba ikulu na jengo la kufanyia UFISADI wa EPA, ESCROW, RICHMOND, n.k.
(a-9) tanzania haikuwa na kiongozi kwa kipindi cha karibu wiki moja kila mwezi, kwa sababu kiongozi wake alikuwa marekani. Safari nyingi kuliko hata zile za kiongozi wa nchi kubwa kama marekani!
(a_10) tanzania ilikuwa na mtu ambaye anafikiri kujenga barabara ya km 60 - maili 25 tu, ni JAMBO kubwa la kujivunia na kutumia mahela mengi ya serikali (zaidi ya zile zilizotumika kujenga barabara hiyo) ETI kwenda kufungua barabara.
Ni hayo mambo kumi tu....mengi yangefikia mia TATU!! Hapakuwepo na kiongozi wa awamu ya nne ndani ya tanzania!!
Mungu ibariki tanzania, tuokoe na Arabu Springs! Nyie wenye nafasi ya kukwapua ndani ya serikali ya ccm, mnaona kwamba ni sawa tu - huo ni ubinafsi. Hii nchi ni ya watanzania wote. Wenye uhalali wa kupata sehemu ya rasilimali zetu pia. Mungu hakutoa rasilimali hizi kwa watu na wadau wa chama kimoja tu. Hamtaendelea kutawala daima. Ndio maana mmepata jeuri hata mnafikia mahali mnatoa maneno ya kejeli kama haya yafuatayp hapa chini:
(a) makapi
(b) goli la mkono
(c) watakiona cha mtema kuni.
shame on you all, who are in the ccm party and those who support the current administration on the pretext of "amani na upendo" ! Shame on you again and again!
Acha umbea wewe hii ndio tatizo kwa watu kama nyinyi hujui demokrasi maana yake nini mkipewa demokrasi hamjui namna ya kuitumia ilihali mmepata uhuru wa kusema kama kweli yote hayo unaya andika unayajua subiri wakati wa kampeni uanze kufoka mpaka jasho la matako likutoke uone kama huyo mtu wako atashinda si kutujazia nzi na lako moja huna
DeleteKama humjui wewe ni pumbafu. Mburura nadhani wote tunamfahamu ila kwa u zito tofauti
ReplyDeleteAende tu washa chukua wengi yeye sio wakwanza na wala hatakuwa wa mwisho goog luck Raisi wa wasafi Ukawa a.k.a Fisadi wazamani wa ccm.
ReplyDeletesalum Mwalimu and Mbatia Ur the great future good leaders
ReplyDeleteTume Cooopy @ SALUM mwalim tiko pamoja wana ukawa na wale wote wenye kiu ya mabadiliko bado milango iko wazi karibun kwenye safari nzuri hiii
Leaders Nikutakieni Hekima Busara katika kipindi muhimu hiki
Salum Mwalimu umefanya kazi nzur sana inaonekana
TEAM LOWASA CDM
Hutaki kapige selfie Mliman city na akina wema na TUTAKUTANA MWISHO WA SAFARI
By De Santos
Lowassa ndie rais wa awamu ya tano.
ReplyDeletekama humjui unafanya nini hapa? labda ukamuulize mama yako anamjua
ReplyDeletelowasa
ReplyDeletekama huku arusha hatuitaki ccm na mkoa umejitambua, sio mikoa iliokumbatia ccm ni maskini watupu
ReplyDeleteUnauliza majibu: Lowassa ni nani. Hujui ni Rais anaesubiri kuapishws?
ReplyDelete