LOWASSA: Tutachukua Nchi Asubuhi Asubuhi 'Hatuko Tayari Kuibiwa Kura'

EDWARD Lowassa ambaye ni mgombea urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema chama hicho kwa ushirikiano na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) watashika dola Oktoba 25 mwaka huu saa 2:30 asubuhi. Anaandika Jimmy Mfuru … (endelea).

Akizungumza na wajumbe wa chama hicho kwenye Mkutano Mkuu leo jijini Dar es Salaam Lowassa amesema, hakuna sababu ya kutoa lugha za matusi huku akiwasihi kuimarishwa kwa amani wakati wa uchaguzi huo.

“Muungano huu una nguvu kubwa ya kwenda kuchukua dola saa 2:30 asubuhi, na tutachukua dola asubuhi,” amesema Lowassa na kuongeza; “hatuko tayari kuibiwa kura na hatutafanya fujo lakini wasiibe kura zetu.”

Amesema kuwa, katika maisha yake hana msamiati wa kushindwa isipokuwa ana msamiati wa kushinda huku akiwataka wana Chadema na UKAWA kuwa wamoja katika kukidondosha Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani.
Lowassa amesema, wakati akiwa CCM safari yake ya kwenda Ikulu ilikuwa ‘Safari ya Matumaini’ na sasa ndani ya Chadema kwa usaidizi wa UKAWA safari hiyo inaitwa ‘Safari ya Mabadiliko nje ya CCM.’

Akiwa mwenye kujiamini amesema, changamoto kubwa ipo katika UKAWA kutokana na walio nje ya umoja huo kwa maana ya CCM kufikiria kuuvuruga.
Hata hivyo ameabainisha kuwa, hatua ya Chadema na UKAWA kumwamini na kumkabidhi bendera ya kupeperusha kwenye Uchaguzi Mkuu ujao ni nzito.

“Kazi miliyonipa ni nzito, nasisitiza kuwa sitawaangusha, nitawajibika kwa vitendo,” amesema Lowassa huku akiwahakikishia wajumbe hao kuwa chama hicho na UKAWA watashika dola.Lowasa ambaye ni Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli amesema, hakukurupuka kufikia uamuzi wa kuhamia Chadema na kwamba, alifanya mashauriano na mkewe pamoja watu wanaomzunguka.
Amesema, “sikujiunga Chadema kwa bahati mbaya, nilikaa na mke wangu, familia yangu pamoja na watu wanaonizunguka na kufikia uamuzi huu. Nasema kuwa, kazi ya chama ni kushika dola na tumejiandaa kushika dola. Nitapita kila jimbo la nchi hii kuhakikisha tunachukua majimbo yote, kajiandaeni huko, nakuja.”

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Utachukua nchi ya nani? Si mpaka uipate. Watu wamehenyeka na kujenga chama, we unakuja kichwakichwa unapewa cheo kirahisi rahisi kisa utajiri wako. Hapa utaisoma namba. Ikulu huipati hata kwa dawa.

    ReplyDelete
  2. Edo Plan ''A'' Umetemwa CCM, Plan ''B'' umepewa fursa UKAWA ujaribu tena bahati yako uingie ikulu ukifeli jaribu Plan ''C'' fanya maamuzi magumu tena omba Monduli ijitawale ujenge ikulu yako huko.

    ReplyDelete
  3. Tuambie ya Richmond na Epa muzeeeeeeeeeeeeeee,mbona hauko wazi?
    Huhusiki na Richmond,sawa,tuambie,tuweke wazi kabla ya october.

    ReplyDelete
  4. Time will tell

    ReplyDelete
  5. Waambie El maana Wanachojua ni kuiba tu

    ReplyDelete
  6. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  7. Hizo ni ndoto za alinacha, eti mtachukua nchi asubuhi, kura zinapigwa usiku??? We'jiandae kuzimia tarehe 27/10/2015 asubuhi, saa ni hiyohiyo uloitaja! Maguli woyeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  8. Edo do expect unexpected you and your PIPI'S POWER as long you have cheated Dr. Slaa

    ReplyDelete
  9. Waambie Edo wote hapo juu ni watoto wa wajumbe wa ccm na Kama si watoto wa wajumbe basi akili zao sio timamu na ni kama vijana walio chini ya miaka 40 wanatakiwa wapelekwe milembe,tanzania inaitaji kuvunja hii system ya mfumo dume wa ccm,nchi inatia aibu miaka 50 baada ya uhuru maji,hospital,umeme hautoshelezi ,halafu mtu mzima na akili yake anashabikia upuuzi wa ccm,hakuna nchi ambayo imewahi kuendelea bila upinzani,unlock your mind you peoples,its for changes,nchi ina madini ya kila aina,vyanzo vyote vya maji lakini hakuna umeme wala maji,kweli mna wazima.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ndio kichaa unaupinga ukweli kubali hata kama unauma ndio maana tunakosa maendeleo kwa kuendekeza ushabiki waki senge jitu hata kama halifai tunaling'ang'ania tu hii kama nchi haina mwenyewe mtu safi mzee Slaa mnamtosa kweli hi sio laana mnamkubali kapi la CCM mmen'gang'ania kuitoa CCM hata kama mnatupeleka jehanamu hatukatai mabadiliko lakini yawe ya kweli sio kwa uchu wetu wa kutaka mabadiliko ndio uwe udhaifu na mwanya wakutumiwa na wenye tamaa ya kuingia ikulu wasio weza kuleta tija yoyote ilihali kaipata ikulu

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad